-
Alkhamisi, tarehe 21 Mei, 2020
May 21, 2020 01:34Leo ni Alhamisi tarehe 27 Ramadhan mwaka 1441 Hijiria, inayosadifiana na tarehe Mosi Khordad mwaka 1399 Hijria Shamsia sawa na 21 Mei mwaka 2020 Miladia.
-
Sisitizo la Russia juu ya kutoweza Marekani kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran
May 19, 2020 02:52Tarehe 8 Mei 2018, Marekani ilijitoa kijeuri katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia yanayojulikana kwa jina maarufu la JCPOA, lakini hivi sasa inafanya njama kubwa za kujaribu kuzuia utekelezaji wa makubaliano hayo hasa kipengee cha kuondolewa Iran vikwazo vya silaha kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo tarehe 18 Oktoba mwaka huu wa 2020. Hata hivyo wajumbe wa Mashariki wa kundi la 4+1 yaani Russia na China wamepinga vikali njama hizo za Marekani.
-
Jumanne, tarehe 19 Mei, 2020
May 18, 2020 21:51Leo ni Jumanne tarehe 25 Ramadhan mwaka 1441 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 19 Mei mwaka 2020 Miladia.
-
Kamati ya Bunge la Iran yaidhinisha muswada dhidi ya utawala wa Kizayuni
May 18, 2020 05:30Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiisalmu (Bunge la Iran) imeidhinisha muswada wa namna ambavyo Iran itakabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika upeo wa kitaifa na kimataifa.
-
Ombi la Umoja wa Mataifa kuhusu kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran
May 17, 2020 02:17Baada ya serikali ya Rais Donald Trump kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) mwaka 2018 katika fremu ya sera za mashinikizo ya juu kabisa na kisha kushadidisha vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika historia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na licha ya kuibuka ugonjwa wa COVID-19 nchini Iran, lakini bado Trump anasisitiza kuendeleza vikwazo vyake vilivyo dhidi ya ubinadamu dhidi ya taifa hili.
-
Marekani ya Trump; nembo na mshirika wa ugaidi wa kiserikali ulimwenguni
May 15, 2020 21:58Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani ni nembo ya ugaidi wa kiserikali na kueleza kwamba, historia ya nchi hiyo katika kuunga mkono ugaidi iko wazi kabisa.
-
Waliopona ugonjwa wa COVID-19 nchini Iran wakaribia 92,000
May 15, 2020 08:02Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari ya Wizara ya Afya ya Iran ametangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa zaidi ya 91,836 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata afueni na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Sayyid Hassan Nasrallah atetea msimamo wa Iran kuhusu mgogoro wa Syria
May 15, 2020 03:03Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ametoa hotuba yenye kukosoa vikali sera za Marekani na utawala Israel kuhusu misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mgogoro wa Syria.
-
Corona; dhihirisho la tabia ya kigaidi ya Marekani dhidi ya taifa la Iran
May 14, 2020 19:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, licha ya kuwa siku zote Marekani inajulikana kuwa ni nchi ya kigaidi, lakini si kwa kiwango hiki cha hata kuzuia bidhaa za afya na tiba zikiwemo dawa kuwafikia watu wa Iran.
-
Ziara ya Pompeo katika ardhi za Palestina na malengo yake kadhaa
May 13, 2020 23:20Uhusiano wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel umepanuka sana kwa namna ambayo haijawahi kutokea katika wakati huu wa urais wa Donald Trump huko Marekani ambaye amechukua hatua nyingi za kutekeleza kivitendo matakwa haramu ya 'Israel.'