-
Iran, Uturuki, Russia na India zaitisha kikao Ankara kuipiga teke sarafu ya dola ya Marekani
Oct 19, 2018 21:39Kikao cha "Changamoto na Fursa za Biashara kwa Fedha za Taifa" kilifanyika jana Ijumaa mjini Ankara Uturuki na kushirikisha maafisa na wataalamu kutoka nchi za Iran, Uturuki, Russia na India.
-
Facebook: Iran na Korea Kaskazini hazijahusika kuiba taarifa za watumiaji wa mtandao wetu
Oct 19, 2018 11:35Shirika la Mtandao wa Kijamii la Facebook limekadhibisha tuhuma kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Korea Kaskazini zimehusika kudukua taarifa za watumiaji wa mtandao huo.
-
Zarif: Vikwazo vipya vya US dhidi ya Iran vinakiuka maamuzi ya ICJ
Oct 18, 2018 10:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani imekubuhu na ni mraibu mkubwa wa kuyawekea mataifa mengine vikwazo, na kwamba vikwazo vipya dhidi ya Tehran ni ukiukaji wa moja kwa moja kwa maamuzi ya hivi karibuni ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ).
-
Misimamo na hatua za upande mmoja za Trump; hatari kwa jamii ya kimataifa
Oct 18, 2018 05:51Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa jamii ya kimataifa inapasa kwa uchache kukabiliana na hatua za Marekani za kukiuka na kuvunja sheria ili kulinda heshima yake.
-
Waziri wa Mafuta wa Iran: Marekani lazima iondoe vikwazo ili bei ya mafuta ishuke
Oct 17, 2018 00:48Bijan Namdar Zangeneh, Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, iwapo Marekani itaiondolea vikwazo Iran, bei ya mafuta katika soko la dunia itapungua na hali ya kuvurugika uthabiti iliyopo katika soko hilo hivi sasa itaondoka.
-
Qassemi: Iran na Afghanistan zina historia kongwe katika uhusiano wa pande mbili
Oct 15, 2018 10:42Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Afghanistan ni jirani muhimu wa Iran na kwamba, historia kongwe iliyoko katika uhusiano wa pande mbili inalazimu nchi hizo kuwa na ushirikiano zaidi katika nyuga mbalimbali.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran aonya kuhusu kuibuka 'Hitler' wapya
Oct 15, 2018 10:11Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kuwa, iwapo dunia itaendelea kufumbia macho ukiukwaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na baadhi ya madola ya kibeberu, basi ijiandae kushuhudia watawala madikteta na makatili kama Adolf Hitler, kiongozi wa zamani wa Kinazi nchini Ujerumani.
-
Iran: Trump ameshindwa ndio maana anazidi kupayuka
Oct 15, 2018 04:24Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, viongozi wa Marekani hasa Donald Trump wanaendelea kushindwa mtawalia mbele ya irada na tadibiri makini ya serikali na taifa la Iran na ndio maana wanazidi kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Tehran.
-
VIDEO: Boti za Kasi za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH zinavyopambana na manuwari za Marekani Ghuba ya Uajemi
Oct 14, 2018 10:47Kwa mara ya kwanza Iran imetoa video inayoonesha boti za kasi za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH zikikaribia manuwari ya kivita ya Marekani katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
-
Uingereza: Kufungamana na JCPOA ni msingi wa uhusiano wetu na Iran
Oct 14, 2018 04:21Balozi wa Uingereza nchini Iran amesema kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kama mapatano ya kimataifa ni msingi wa uhusiano wa London na Tehran.