Iran: Trump ameshindwa ndio maana anazidi kupayuka
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i48807-iran_trump_ameshindwa_ndio_maana_anazidi_kupayuka
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, viongozi wa Marekani hasa Donald Trump wanaendelea kushindwa mtawalia mbele ya irada na tadibiri makini ya serikali na taifa la Iran na ndio maana wanazidi kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Tehran.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 15, 2018 04:24 UTC
  • Iran: Trump ameshindwa ndio maana anazidi kupayuka

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, viongozi wa Marekani hasa Donald Trump wanaendelea kushindwa mtawalia mbele ya irada na tadibiri makini ya serikali na taifa la Iran na ndio maana wanazidi kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Tehran.

Bahram Qassemi amesema hayo kujibu matamshi ya hivi karibuni ya rais wa Marekani na mshauri wake wa usalama wa taifa na vile vile sehemu ya hati ya kiistratijia ya kukabiliana na ugaidi ya Marekani. Viongozi wa Marekani wameendelea kutoa madai yao ya kila siku ya kwamba eti Iran inaunga mkono ugaidi. Akijibu madai hayo yasiyo na mashiko, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kutoa tuhuma zisizo na msingi na kurejelewa ndoto za kipuuzi katika hotuba za viongozi wa Marekani hususan za rais wa nchi hiyo kunatokana na kushindwa mfulilizo Washington katika miezi ya hivi karibu kwenye nyuga tofauti za kukabiliana na imani thabiti, muqawama na tadibiri makini ya Iran na Wairani.

Trump katika ndoto za mchana za Alinacha

 

Amesema, walichokiona walimwengu katika kikao cha hivi karibuni cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na pia katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo, ni mlolongo wa kuzidi kususiwa siasa za kujikumbizia upande mmoja za Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, Wamarekani wanafanya njama za kupotosha walimwengu na kujaribu kuwasahaulisha historia ya umwagaji damu, ukatili na kuchochea vita na machafuko kunakofanywa na Marekani katika kona zote za dunia likiwemo eneo la Mashariki ya Kati.