-
"Chuki dhidi ya Uislamu ni chombo cha kuhalalisha jinai za Israel"
Mar 15, 2025 03:36Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani mwenendo unaoongezeka wa kueneza chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu duniani na kusema kuwa, chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ni nyenzo ya kuhalalisha uvamizi na jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Wataalamu wa UN waituhumu Israel kwa udhalilishaji wa kingono dhidi ya Wapalestina
Mar 14, 2025 11:28Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameituhumu Israel kuwa imewadhalilisha kingono na kijinsia Wapalestina wakati wa vita na mauaji ya kimbari ya utawala huo dhidi ya wakazi wa Gaza.
-
Hizbullah: Muqawama uliilazimisha Israel kukubali usitishaji vita
Mar 10, 2025 07:56Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah amesema Israel ilikubali kusitisha mapigano na Lebanon baada ya kupata vipigo vikali kutoka kwa wapiganaji shupavu wa Muqawama.
-
Russia: Israel haina haki ya kuzungumzia miradi ya nyuklia ya Iran
Mar 08, 2025 00:54Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Mashirika ya Kimataifa mjini Vienna, Mikhail Ulyanov, amesema kuwa utawala wa Israel hauna haki ya kutoa maoni kuhusiana na mpango wa amani wa nyuklia wa Iran.
-
Askari wa Israel wavamia misikiti mjini Nablus na kuzuia Swala ya Ijumaa
Mar 07, 2025 07:31Vikosi vya jeshi la Israel vimevamia misikiti kadhaa katika mji mkongwe wa Nablus, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kuzuia kuswaliwa Swala ya Ijumaa.
-
Jeshi la Israel launda kifaa cha AI cha kuwajasisi Wapalestina
Mar 07, 2025 07:27Uchunguzi mpya umefichua kuwa, kitengo cha ujasusi wa kielektroniki cha jeshi la Israel cha 8200 kimetumia mkusanyiko mkubwa wa mawasiliano yaliyonaswa kutengeneza chombo cha kijasusi cha Akili Mnemba (AI) ambacho modeli yake inashabihiana na ChatGPT, kwa lengo la kuwachunguza na kuwafanyia ujasusi wananchi wa Palestina.
-
Amnesty yataka kuchunguzwa jinai za kivita za Israel nchini Lebanon
Mar 05, 2025 22:56Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa mwito wa kufanyika uchunguzi huru juu ya mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya vituo vya matibabu, magari ya dharura na wafanyakazi wa afya nchini Lebanon, na kutaja hujuma hizo kama uhalifu wa kivita.
-
Misaada ya kijeshi na silaha ambayo haijawahi kutolewa mfano wake ya serikali ya Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Mar 03, 2025 23:28Sambamba na Marekani kukata misaada yake kwa Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, siku ya Jumapili alitumia mamlaka ya dharura aliyonayo kisheria kupitisha mpango wa utoaji msaada wa shehena ya silaha zenye thamani ya dola bilioni 4 kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kuendelea hatua za kimataifa dhidi ya uvamizi wa Israel
Mar 02, 2025 22:52Katika kuendeleza mapambano na kupinga jinai za Israel dhidi ya Wapalestina, viongozi wa Afrika Kusini, Malaysia na Colombia wametangaza kuwa watazizuia meli zilizobeba silaha kwa ajili ya Israel kuingia katika bandari za nchi hizo.
-
Ansarullah: Israel inatumia uungaji mkono wa US kukiuka makubaliano
Mar 01, 2025 03:43Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Yemen inafuatilia kwa karibu utekelezwaji wa makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa, inashuhudia namna "adui Mzayuni" anakwepa kutekeleza majukumu yake.