-
Israel inaiangamiza Palestina kielimu kwa kulenga wasomi na vituo vya kielimu Gaza
Jan 22, 2024 04:00Utawala wa Kizayuni wa Israel umewauwa maprofesa 94 wa vyuo vikuu, mamia ya walimu, na maelfu ya wanafunzi katika Ukanda wa Gaza katika muda wa miezi mitatu, kwa mujibu wa shirika moja huru la kutetea haki za binadamu.
-
Hizbullah yazima uvamizi wa kijeshi wa Israel kusini ya Lebanon
Jan 22, 2024 03:59Wanajihadi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wametibua uvamizi wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu, huku ngome za utawala huo ghasibu zikiendelea kulengwa kwa makombora ya kundi hilo la muqawama, likiwa ni jibu kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Wazayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS: Shambulio la Oktoba 7 ilikuwa "hatua ya lazima" dhidi ya ukaliaji ardhi kwa mabavu wa Israel
Jan 22, 2024 00:17Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, shambulio la tarehe 7 Oktoba 2024 dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel lilikuwa "hatua ya lazima" dhidi ya ukaliaji ardhi kwa mabavu unaofanywa na utawala huo dhalimu katika maeneo ya Palestina.
-
Waliouawa shahidi Gaza wapindukia 25,000, Israel yaendeleza mashambulizi ya kinyama
Jan 21, 2024 10:09Maafisa wa Palestina katika Ukanda wa Gaza wametangaza kuwa, wakati vita angamizi vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Gaza vimeingia katika siku yake ya 107 leo, hadi sasa Wapalestina 25,105 wameshauawa shahidi na 62,681 wamejeruhiwa.
-
Marekani: Israel imeshindwa kufikia lengo la vita, HAMAS ingali iko imara, ina silaha za kutosha
Jan 21, 2024 09:18Mashirika ya intelijensia ya Marekani yamesema, idadi ya vifo vya wapiganaji wa harakati ya HAMAS vilivyotokana na uvamizi unaoendelea wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza haifikii lengo la utawala huo la kulitokomeza kundi hilo la muqawama wa Palestina.
-
New York Times: Iran imetuma ujumbe kwa Israel kwa kombora la Khaybar-Shekan
Jan 20, 2024 09:04Gazeti la Marekani la New York Times limelitaja shambulio la hivi karibuni la makombora ya Iran dhidi ya ngome za kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) nchini Syria kwa kutumia kombora la kisasa la "Khaybar Shekan" kuwa sio tu ni kulipiza kisasi dhidi ya ISIS bali pia ni onyesho la nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya kambi ya Magharibi na hasa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
UN: Maelfu ya Wapalestina wa Gaza waliokamatwa na askari wa Israel wanateswa
Jan 20, 2024 03:52Umoja wa Mataifa umesema huenda vikosi vya jeshi la Israel vimewakamata maelfu ya Wapalestina wakazi wa Ukanda wa Gaza, huku utawala huo wa Kizayuni ukiendeleza mauaji na jinai za kutisha dhidi ya wakazi wa eneo hilo uliolizingira.
-
Mtaalamu wa UN: Hakuna kinachoweza kuhalalisha ilichokifanya Israel Gaza
Jan 19, 2024 08:17Mtalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameashiria ukiukaji wa sheria za kimataifa uliofanywa mara chungu nzima na utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, hakuna kitu kinachoweza kuhalalisha vita vya mauaji ya kimbari vya Israel katika eneo hilo lilozingirwa.
-
Mexico na Chile zaitaka ICC ichunguze jinai za Israel Gaza
Jan 19, 2024 08:16Serikali za Mexico na Chile zimeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuchunguza na kuwashtaki maafisa wa utawala wa Israel ambao wamehusika katika jinai za kivita dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Indhari ya Uhispania kuhusu matukio ya eneo na ya kimataifa ya vita vya Gaza
Jan 18, 2024 23:57Pedro Sánchez, Waziri Mkuu wa Uhispania ameonya kuwa, usalama na uthabiti wa eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) umekuwa hatarini na kwamba, mashambulizi haya yanahatarisha nidhamu na uratibu wa ushirikiano wa pande kadhaa.