-
Kesi ya Afrika Kusini dhidi ya uhalifu wa Israel huko Gaza katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Jan 18, 2024 08:38Makaka yetu wiki hii itaangazia mashtaka yaliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, (IJC) kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza huko Palestina.
-
Himaya mpya ya Magharibi kwa Israel
Jan 18, 2024 05:05Wakati ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel bado unaendeleza mauaji yake dhidi ya Wapalestina wa Gaza, nchi za Magharibi nazo zinaendelea kutoa himaya na misaada kwa utawala huo, na kinyume na madai yote ya eti kutetea haki za kibinadamu yanayotolewa na nchi hizo, zinaiwezesha Israel kuendeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.
-
Malaysia: Magharibi ni mshirika wa jinai za Israel kwa kimya chake
Jan 17, 2024 04:12Waziri Mkuu wa Malaysia amezikosoa vikali nchi za Magharibi kwa kuendelea kufumbia macho matukio ya Gaza na kusisitiza kuwa, Wamagharibi ni washirika wa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina kwa kimya chao hicho.
-
Marekani yatiwa kiwewe na shambulio la IRGC dhidi ya kituo cha Mossad
Jan 16, 2024 23:08Maafisa wa Marekani wameghadhabishwa mno na hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) kufanya shambulio la makombora dhidi ya kituo kikuu cha ujasusi cha shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel Mossad katika eneo la Kurdistan ya Iraq.
-
Afrika Kusini kuzishtaki Marekani na Uingereza kwa kuhusika na jinai za kivita za Israel Gaza
Jan 16, 2024 03:35Baada ya Afrika Kusini kuwasilisha kesi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa kuhusika na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza, mawakili wapatao 50 wa nchi hiyo wanatayarisha mashtaka mengine tofauti dhidi ya serikali za Marekani na Uingereza kwa msingi kwamba, serikali hizo zinahusika katika jinai na uhalifu unaofanywa na jeshi la Israel huko Gaza.
-
Kuongezeka hitilafu katika serikali ya Biden kuhusiana na vita vya Gaza
Jan 15, 2024 23:15Sambamba na uendelea vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu madhulumu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina, kuzidi kuzorota hali ya mambo katika eneo la Magharibi mwa Asia na himaya ya wazi na ya siri ya Marekani kwa utawala huo ghasibu, ushahidi uliopo unaonyesha kuwa hali inazidi kuwa ngumu kwa Marekani siku baada ya siku kutokana na kuendelea kuunga mkono jinai za Israel, hasa mauaji ya halaiki ya Wapalestina.
-
Namibia yaikumbusha Ujerumani kwamba ilifanya mauaji ya kwanza ya kimbari ya karne ya 20
Jan 14, 2024 09:43Namibia imepinga uungaji mkono wa Ujerumani kwa msimamo wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, (ICJ) ambapo inakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Walimwengu waandamana kulaani siku 100 za jinai za Israel Gaza
Jan 14, 2024 00:02Mamilioni ya watu jana Jumamosi walifanya maandamano katika pembe mbali mbali za dunia kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na vile vile kuonyesha mshikamano wao na taifa la Palestina.
-
Juhudi za utawala wa Kizayuni za kupotosha uhakika wa kutisha wa vita vya Gaza
Jan 13, 2024 08:46Kikao cha kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, yenye makao yake huko Hague Uholanzi kimeanza katika hali ambayo mauaji ya kimbari na jinai za kivita za utawala wa Israel unaoiklia Quds kwa mabavu zingali zinaendelea katika ardhi za Palestina; na kila siku wananchi wa Palestina wanaendelea kuuliwa shahidi.
-
Kuanza kusikilizwa mashtaka ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya utawala wa Kizayuni
Jan 11, 2024 23:11Mahakama ya Kimataifa ya Haki yenye makao makuu yake mjini The Hague Uholanzi Alhamisi na Ijumaa inasikiliza na kukusanya mitazamo ya kisheria ya Afrika Kusini na utawala wa Kizayuni kuhusu kesi ya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza. Moja ya shughuli za mahakama hiyo ni kushughulikia mashtaka yanayohusiana na Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa 1948. Mkataba huo unatambuliwa rasmi na nchi 153.