-
Watu 50 wauawa katika shambulio la ADF mkoani Ituri, DRC
May 31, 2021 22:45Kwa akali watu 50 wameuawa katika shambulio la kundi la wanamgambo wa ADF dhidi ya vijiji viwili mashariki mwa mkoa wa Ituri huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Wacongo waliokimbia volcano Goma wanasumbuliwa na ubaha wa chakula, maji
May 29, 2021 07:42Wakazi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) waliokimbia makazi na nyumba zao Jumamosi iliyopita kutokana na mlipuko wa volkano ya Mlima Nyiragongo ambao wanahofia kutokea mlipuko mwingine wa volkano, wasumbuliwa na uhaba wa chakula na maji.
-
Asilimia 5 ya wabunge wa Congo DR wamefariki dunia kwa virusi vya corona
May 28, 2021 23:51Makamu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema wabunge 32 ambao ni sawa na karibu asilimia 5 ya jumla ya wabunge wote wa nchi hiyo, wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 tangu kuanza kwa janga hilo.
-
Watu wasiopungua 15 wafariki dunia, mamia ya nyumba yateketea, volcano ya Goma
May 24, 2021 03:32Watu karibu 15 wamethibitishwa kufariki dunia kutokana mlipuko wa volkano uliotokea katika Mlima wa Nyiragongo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
-
30 wahukumiwa kifo Congo DR kwa kuhusika na ghasia za siku ya Idul Fitri
May 15, 2021 09:55Watu thelathini wamehukumiwa kifo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kesi isiyosikilizwa katika siku moja tu, kwa kupatikana na hatia ya kuhusika na ghasia dhidi ya polisi wakati wa ibada ya Swala ya Idul Fitri ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani katika mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Wanamgambo 10 wa ADF waangamizwa na jeshi la Kongo DR
May 10, 2021 22:21Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza habari ya kuwauwa wanamgambo wasiopungua 10 wa ADF mashariki mwa nchi, katika operesheni dhidi ya genge hilo la wapiganaji.
-
ICC yamhukumu Ongwen kifungo cha miaka 25 jela
May 06, 2021 08:12Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wamemhukumu kifungo cha miaka 25 jela Dominic Ongwen, mwanajeshi mtoto wa zamani wa Uganda ambaye alikuwa kamanda wa kundi la waasi wa Lords Resistance Army (LRA), baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu nchini Uganda.
-
DRC yadhibiti mripuko wa 12 wa ugonjwa wa Ebola
May 03, 2021 21:03Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza habari ya kudhibitiwa mripuko wa 12 wa ugonjwa wa Ebola nchini humo, miezi mitatu baada ya kesi ya kwanza kuripotiwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
-
DRC yatangaza 'hali ya mzingiro' katika mikoa ya mashariki
May 01, 2021 08:08Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza 'hali ya mzingiro' katika mikoa miwili ya mashariki mwa nchi inayoshuhudia mapigano na umwagaji damu kwa miezi kadhaa sasa.
-
23 wauawa katika mauaji mengine ya halaiki Mashariki mwa Congo DR
Mar 31, 2021 22:32Afisa mmoja wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa watu waliokuwa na silaha ambao wanadhaniwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) kutoka Uganda wameua raia wasiopungua 23 huko Mashariki mwa nchi hiyo.