May 19, 2020 07:22
Tarehe 8 Mei 2018, Marekani ilijitoa kijeuri katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia yanayojulikana kwa jina maarufu la JCPOA, lakini hivi sasa inafanya njama kubwa za kujaribu kuzuia utekelezaji wa makubaliano hayo hasa kipengee cha kuondolewa Iran vikwazo vya silaha kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo tarehe 18 Oktoba mwaka huu wa 2020. Hata hivyo wajumbe wa Mashariki wa kundi la 4+1 yaani Russia na China wamepinga vikali njama hizo za Marekani.