Jan 11, 2020 08:13
Katika zama za utawala wa Rais Donald Trump, serikali ya Marekani imekuwa ikifuatilia sera za mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Iran na katika fremu hiyo mnamo Mei 8 2018, Washington ilitangaza kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na baada ya hapo ikaweka vikwazo shadidi zaidi dhidi ya Iran. Pamoja na kuwa vikwazo hivyo havijafikia malengo yaliyokusudiwa, Marekani inasisitiza kuendeleza sera yake ya kushadidisha vikwazo.