Umoja wa Mataifa wasisitiza kudumishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
(last modified Wed, 15 Jan 2020 12:40:36 GMT )
Jan 15, 2020 12:40 UTC
  • Umoja wa Mataifa wasisitiza kudumishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

Umoja wa Mataifa umezitaka pande zote husika katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) kufanya kila ziwezalo kuhakikisha kwamba, zinayadumisha makubaliano hayo muhimu ya kimataifa.

Wito huo umetolewa Stéphane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa  ambaye hakuashiria hatua ya serikali ya Marekani ya kujitoa katika makubaliano hayo ambayo inatajwa kuwa sababu ya mkwamo wa makubaliano hayo na badala yake amesisitiza tu kwamba, kuna haja kwa makubaliano hayo kudumishwa.

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa ameitaka Iran iendelee kushirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomikia (IAEA) sambamba na kutekeleza kikamilifu ahadi na majukumu yake kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Stéphane Dujarric amesema hayo baada ya nchi tatua za Ulaya kuanzisha mchakato wa kutatua hitilafu ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA, hatua ambayo imetajwa na Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran kwamba, ni kosa la kiistratijia.

Dakta Zarif sambamba na kuzlaumu nchi tatu za Ulaya za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwa uamuzi wao usio na sababu wa kuanzisha mchakato wa kutatua hitilafu ndani ya JCPOA baada ya nchi hizo kushindwa kutekeleza ahadi zao kutokana na mashinikizo ya Marekani ameeleza kuwa, hoja zilizotolewa na nchi hizo katika hatua yao hiyo hazina mashiko ya kisheria, na ni kosa la kiistratijia katika upande wa kisiasa.

Tags