Nov 29, 2019 06:57
Hatua ya Iran kupunguza utekelezaji wa ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) imekabiliwa na ukosoaji mkali wa nchi za Ulaya katika kundi la 4+1 ambalo linazileta pamoja China, Russia, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani. Ifahamike kuwa, Iran imechukua hatua hiyo baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya JCPOA na nchi za Ulaya kushindwa kuchukua hatua za kivitendo za kufidia Marekani kujiondoa katika mapatano hayo ya kimataifa ya nyuklia.