Nov 07, 2019 10:40
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameliagiza Shirika la Nishati ya Atomiki (IAEO) lianze kuingiza gesi kwenye mashinepewa (centrifuges) katika kituo cha nyuklia cha Fordow, ikiwa ni katika utekelezaji wa hatua ya nne ya kupunguza uwajibikaji wa Tehran katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.