Rouhani: Maadui wanadhani watausambaratisha Mfumo wa Kiislamu kwa kuhujumu JCPOA
(last modified Thu, 24 Oct 2019 02:49:59 GMT )
Oct 24, 2019 02:49 UTC
  • Rouhani: Maadui wanadhani watausambaratisha Mfumo wa Kiislamu kwa kuhujumu JCPOA

Rais Hassan Rouhani amewashangaa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanaodhani kuwa, kwa kuhujumu na kukiuka makubaliano ya nyuklia ya JCPOA watausambaratisha Mfumo wa Kiislamu hapa nchini.

Rais Rouhani alisema hayo jana Jumatano katika mkutano wa Baraza la Mawaziri na kuongeza kuwa, maadui walikuwa na ndoto za alinacha kuwa wangefanikiwa kuvuruga mfumo wa kisiasa hapa nchini kwa kuidhalilisha JCPOA, lakini taifa la Iran limesimama kidete na haliweze kurubuniwa na adui.

Ameeleza bayana kuwa, "Wananchi wa Iran wanawafahamu vyema wanaowadhulumu na wanaokiuka makubaliano ya JCPOA; na wanatambua athari na manufaa ambayo yangeletwa nayo."

Dakta Rouhani amebainisha kuwa, "JCPOA ilionesha ni namna gani diplomasia komavu, mienendo na irada ya kisiasa ya taifa hili inaweza kuwa athirifu. Ni kwa sababu hii ndiyo maana utawala wa Kizayuni, Saudi Arabia na Wamarekani wenye misimamo mikali wasingeweza kuyavumilia mapatano hayo."

Rais Rouhani katika mkutano wa Baraza la Mawaziri

Kadhalika amesisitiza kuwa serikali yake inaona fahari kubwa na itaendelea kupambana kwa dhati na ugaidi na ufisadi kwa maslahi ya taifa hili.

Rais Hassan Rouhani ameongeza kuwa, nchi hii itaendelea kuimarisha uhusiano na nchi nyingine za dunia ili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara wa pande mbili na pande kadhaa.

 

Tags