-
Qassemi: Iran haijapokea pendekezo la JCPOA kutoka Umoja wa Ulaya
Jun 30, 2018 11:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria habari kuwa Umoja wa Ulaya umewasilisha pendekezo la kuunga mkono mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana rasmi kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji, (JCPOA), na kusema, "hadi sasa Iran haijapokea kifurushi cha mapendekezo kutoka Umoja wa Ulaya."
-
Mogherini: EU imekipigia kura ya ndio kifurushi cha kuiunga mkono Iran kuhusiana na JCPOA
Jun 29, 2018 23:55Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini amesema kuwa umoja huo umekipigia kura 28 za ndio kifurushi cha kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika fremu ya makubaliano ya nyuklia maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
-
Russia: Pande zote ndani ya JCPOA zijawajibike kuyalinda makubaliano hayo
Jun 29, 2018 11:00Mwakilishi wa Russia katika Taasisi za Kimataifa mjini Vienna Austria amesema kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni muhimu sana na kwamba nchi zilizosalia katika makubaliano hayo zinapasa kuyalinda.
-
Russia yasisitiza kwa mara nyingine kuwa hakuna mbadala wa mapatano ya nyuklia ya Iran, JCPOA
Jun 29, 2018 00:16Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia kwa mara nyingine imesisitiza kuwa nchi hiyo inaunga mkono mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji, JCPOA.
-
Rouhani: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imevuka njama za adui
Jun 26, 2018 10:16Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia njama zinazofanywa na Marekani dhidi ya Iran tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na kkusema kuwa, taifa na mfumo wa Iran umevuka njama za adui katika vipindi mbalimbali kutokana na kuwa macho na makini.
-
Iran: Mapatano ya nyuklia ya JCPOA bado yako hai
Jun 25, 2018 10:25Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, licha ya kwamba Marekani imejitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA lakini makubaliano hayo ya kimataifa bado yako hai na mazungumzo juu ya namna ya kuendeleza ushirikiano kupitia mapatano hayo yangali yanaendelea.
-
Iran: Reuters inaeneza habari 50 za uongo kila siku dhidi yetu; uanagenzi wa Trump ni kwa manufaa ya Tehran
Jun 24, 2018 10:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria hatua zisizo za kimantiki za rais wa Marekani ikiwa ni pamoja na uamuzi wake wa kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, matokeo ya hatua hizo ni kuzidi kuharibika jina la Donald Trump na kuzidi kunufaika Iran.
-
Araqchi: JCPOA ipo katika ICU, yumkini Iran ikajiondoa wiki chache zijazo
Jun 23, 2018 02:51Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita za kundi la 5+1 maarufu kama JCPOA yako chumba cha wagonjwa mahututi ICU, na yumkini Tehran ikajiondoa kwenye mapatano hayo ndani ya wiki chache zijazo.
-
UN: Kulindwa JCPOA kuna umuhimu kwa usalama wa dunia
Jun 20, 2018 02:59Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kulindwa makubaliano ya nyuklia ya Iran ni jambo lenye udharura mkubwa hususan katika kudhamini usalama wa dunia.
-
Boroujerdi: Matamshi ya nchi za Ulaya kuhusu JCPOA si utatuzi wa matatizo ya Iran
Jun 17, 2018 22:02Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, matamshi chanya ya viongozi wa nchi za Ulaya kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA hayawezi kutatua matatizo ya Iran bali viongozi hao wanapaswa kuakisi misimamo yao kivitendo na watekeleze ahadi zao kwa kutokubaliana na misimamo ya Marekani.