Russia: Pande zote ndani ya JCPOA zijawajibike kuyalinda makubaliano hayo
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46440-russia_pande_zote_ndani_ya_jcpoa_zijawajibike_kuyalinda_makubaliano_hayo
Mwakilishi wa Russia katika Taasisi za Kimataifa mjini Vienna Austria amesema kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni muhimu sana na kwamba nchi zilizosalia katika makubaliano hayo zinapasa kuyalinda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 29, 2018 11:00 UTC
  • Russia: Pande zote ndani ya JCPOA zijawajibike kuyalinda makubaliano hayo

Mwakilishi wa Russia katika Taasisi za Kimataifa mjini Vienna Austria amesema kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni muhimu sana na kwamba nchi zilizosalia katika makubaliano hayo zinapasa kuyalinda.

Mikhael Ulyanov amebainisha kuwa makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya kundi la 5+1 na Iran yanang'ara na kwamba Russia inataraji kuwa, pande zote zitafungamana na kutekeleza majukumu yao kuhusiana na makubaliano hayo.  

Ulyanov ameongeza kuwa, suala la kufanyika kikao cha mawaziri wa nchi zilizoshiriki katika makubaliano hayo ya nyuklia limewekwa katika ajendai na kwamba kwanza kabisa Iran inataka kujua ni hatua zipi zitachukuliwa na nchi wanachama wa makubaliano ya JCPOA kwa ajili ya kufidia madhara yaliyosababishwa na kujitoa Marekani katika makubaliano hayo.

Alhamisi wiki hii Sergei Ryabkov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia pia alisema kuwa nchi zilizoshiriki katika makubaliano hayo ya nyuklia zinapasa kusisitiza kuwa makubaliano  hayo ya kimataifa hanafungamani na maamuzi ya kisiasa ya Marekani. 

Sergei Ryabkov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia 

Itakumbukwa kuwa Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 8 mwezi Mei mwaka huu alikariri tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Iran na kutangaza kwamba, Washington imejiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA sambamba na kurejeshwa vikwazo vya nyuklia katika kipidi cha miezi mitatu hadi sita. Baada ya kujitoa huko kwa Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia ilitoa muhula kwa pande husika katika makubaliano hayo yaani Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, China na Russia zibuni utaratibu wa kudhamini na kulinda maslahi ya Iran katika mapatano hayo.