-
Russia yapinga matamshi ya Trump, Macron kuhusu makubaliano ya JCPOA
Apr 26, 2018 23:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amepinga matamshi yaliyotolewa na Marais wa Marekani na Ufaransa kuhusu suala la kufanyiwa mabadiliko makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Azma ya kimataifa kwa ajili ya kulinda mapatano ya JCPOA
Apr 26, 2018 08:41Huku tarehe 12 Mei ikiwa inakaribia, ambayo ni tarehe ya mwisho iliyoainishwa na Rais Donald Trump wa Marekani kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi sita kubwa za dunia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA, radiamali na harakati za serikali na viongozi wa kundi la 5+1 kwa ajili ya kulinda mapatano hayo zimeongezeka.
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka mapatano ya nyuklia ya Iran yalindwe
Apr 26, 2018 03:24Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) yanapaswa kulindwa.
-
Zarif: Iran itafuata nyayo iwapo US itajiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia
Apr 25, 2018 03:04Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuna uwezekano mkubwa Iran itajiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, iwapo Marekani itaamua kujivua kwenye mapatano hayo ya kimataifa ya mwaka 2015.
-
Shamkhani: Marekani na Ulaya zikivuka mstari mwekundu wa Iran zitagonga mwamba
Apr 24, 2018 22:02Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa nchini Iran amesema kuwa, iwapo Ulaya itafanya makosa ya kistratijia na kusalimu amri mbele ya Marekani na kuvuka mistari mnyekundu ya Iran kwa shabaha ya kutaka kumridhisha Donald Trump, hapana shaka kuwa itakula mweleka na kushindwa.
-
Rais Rouhani aonya kuhusu taathira hasi iwapo JCPOA itakiukwa
Apr 24, 2018 12:04Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameionya Marekani dhidi ya kukiuka makubaliano ya nyuklia ya Vienna na kusisitiza kuwa, endapo Washington itajiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa kama inavyotishia, basi hatua hiyo itakuwa na matokeo mabaya.
-
Matakwa ya taasisi za kimataifa kwa Marekani kuhusu mapatano ya nyuklia ya Iran
Apr 24, 2018 05:39Wakati wa rais wa Marekani Donald Trump wa kuchukua maamuzi kuhusu mapatano ya nyuklia ya Iran unazidi kukaribia katika hali ambayo jamii ya kimatiafa imeongeza jitihada za kumlazimisha aheshimu vipengee vya mapatano hayo ambayo Marekani ilishiriki kikamilifu kuyafanikisha.
-
UN yazitaka pande zote husika kuheshimu na kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Apr 23, 2018 22:47Mkuu wa idara ya udhibiti silaha ya Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa pande zote husika katika makubaliano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kuheshimu na kutekeleza makubaliano hayo.
-
Iran: Marekani ikijitoa katika JCPOA, tutaanzisha tena shughuli za nyuklia kwa kiwango cha kisasa zaidi
Apr 23, 2018 00:09Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, chaguo kuu la Iran endapo Marekani itajitoa katika makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA ni kuanzisha tena shughuli za nyuklia za taifa hili zenye malengo ya amani lakini kwa kiwango cha juu na cha kisasa zaidi.
-
Macron: Ufaransa haina mpango mwingine mbadala wa makubaliano ya JCPOA
Apr 22, 2018 23:32Rais wa Ufaransa ameashiria kuwa Paris haina mpango mwingine mbadala wa makubaliano ya JCPOA na kuitaka Marekani isalie katika makubaliano hayo ya pamoja na Iran.