Macron: Ufaransa haina mpango mwingine mbadala wa makubaliano ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i43520-macron_ufaransa_haina_mpango_mwingine_mbadala_wa_makubaliano_ya_jcpoa
Rais wa Ufaransa ameashiria kuwa Paris haina mpango mwingine mbadala wa makubaliano ya JCPOA na kuitaka Marekani isalie katika makubaliano hayo ya pamoja na Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 22, 2018 23:32 UTC
  • Macron: Ufaransa haina mpango mwingine mbadala wa makubaliano ya JCPOA

Rais wa Ufaransa ameashiria kuwa Paris haina mpango mwingine mbadala wa makubaliano ya JCPOA na kuitaka Marekani isalie katika makubaliano hayo ya pamoja na Iran.

Akizungmza na kanali ya habari ya Fax News ya nchini Marekani, Rais Emmanuel Macron amebainisha kuwa hakuna mpango mbadala wa kuchukua nafasi ya makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya kundi la 5+1 na Iran na kwamba Marekani inapasa kusalia katika makubaliano hayo madamu hakuna chaguo jingine lililo bora.  

Akiendelea na mahojiano hayo, Rais Macron ametoa madai ya uongo kuhusu matukio ya Syria bila ya kuashiria shambulio la kijeshi la Marekani, Uingereza na nchi yake dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu ambapo amedai kuwa: Marekani na waitifaki wake wana nafasi muhimu katika kuijenga upya Syria baada ya vita. 

Macron ametoa madai hayo katika hali ambayo nchi za Magharibi katika miaka ya karibuni zimeisambaratisha nchi hiyo na kupelekea mamilioni ya watu kuuawa na kuwa wakimbizi na sasa zinatoa madai hayo ya kuijenga upya Syria. Marekani na waitifaki wake  wa Magharibi na wa Kiarabu ndio wameyaingiza huko Syria makundi ya kigaidi na kuyaunga mkono kwa hali na mali. 

Vita vilivyoiathiri Syria kutokana na uungaji mkono wa Marekani na waitifaki wake kwa  makundi ya kigaidi