-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Vikosi vyetu vya Ulinzi havimuogopi adui yeyote yule
Apr 29, 2018 10:41Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iko imara katika kuimarisha uwezo wake wa kuzuia mashambulizi na kusisitiza kwamba, taifa la Iran hususan Vikosi vyake vya Ulinzi havimuogopi adui yeyote yule.
-
Jeshi la Iran lasema haliwezi kupigishwa magoti na maadui
Apr 23, 2018 03:31Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katu Iran haiwezi kupigishwa magoti na kukubali matakwa ya maadui wa taifa hili wakiongozwa na Marekani na waitifaki wake.
-
Magaidi elfu tano (5000) walazimika kuondoka katika viunga vya mji mkuu wa Syria
Apr 18, 2018 22:33Hatimaye, genge la kigaidi la Jeish al Islam limetangaza kuwa limekubali kuondoa wanamgambo wake 5,000 waliko katika eneo la al Dhamir katika viunga vya mji mkuu wa Syria Damascus na kuwapelekea Jarabulus mkoani Halab (Aleppo) pamoja na familia zao.
-
Iran yaonyesha uwezo wake mkubwa wa kijeshi katika Siku ya Taifa ya Jeshi
Apr 18, 2018 03:21Rais Hassan Rouhani amesema uwezo mkubwa wa kijeshi na kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwa ajili ya kujihami na wala sio kwa sababu ya kuivamia nchi yeyote au kudhuru maslahi yao.
-
Baada ya kufurushwa magaidi, wakimbizi 59 elfu warejea makwao Ghouta Mashariki nchini Syria
Apr 16, 2018 03:33Kituo cha Russia cha kusimamia mapatano nchini Syria kimesema kuwa, zaidi ya watu 59 elfu wamerejea katika maeneo yao huko Ghouta Mashariki baada ya kutimuliwa magaidi katika eneo hilo.
-
Jeshi la Syria lateka na kuwashikilia wanajeshi vamizi wa Uingereza Ghouta Mashariki
Apr 11, 2018 22:02Shirika rasmi la habari la Syria limetangaza kuwa wanajeshi kadhaa wa Uingereza wanashikiliwa mateka kufuatia operesheni iliyofanywa na jeshi la Syria huko Ghouta Mashariki katika viunga vya Damascus.
-
Rais wa Ghana: Hatutairuhusu Marekani ijenge kituo cha kijeshi nchini
Apr 06, 2018 23:22Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana amesema nchi hiyo katu haitasaini mkataba na Marekani wa kuiruhusu Washington ijenge kituo cha kijeshi katika nchi hiyo ya Kiafrika.
-
Jeshi la Syria latangaza rasmi kukombolewa kikamilifu Ghouta Mashariki
Apr 01, 2018 02:59Jeshi la Syria limetangaza habari ya kukomboa kikamilifu eneo la Ghouta Mashariki, viungani mwa mji mkuu Damascus.
-
Jeshi la Chad lapambana na magaidi wa Boko Haram
Mar 24, 2018 21:51Duru za kijeshi za Chad zimetangaza habari ya kutokea mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na magaidi wa Boko Haram katika eneo la Ziwa Chad.
-
Israel: Tumepoteza uwezo wetu mkubwa mbele ya harakati ya Hizbullah na Hamas
Mar 03, 2018 01:38Kamanda wa vikosi vya ardhini vya utawala haramu wa lsrael amekiri kwamba, jeshi la utawala huo limepoteza uwezo wake mkubwa mkabala wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon na Harakati ya muqawama wa Palestina HAMAS.