-
Johnson & Johnson yashtakiwa Kenya kwa kuwauzia watu poda iliyopigwa marufuku Ulaya, Marekani
Jun 13, 2023 12:16Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Kenya limeshtaki shirika la kimataifa la Marekani, Johnson & Johnson, kwa kosa la kuwauzia Wakenya poda ya ulanga.
-
Viongozi wa Igad wanakutana leo Djibouti kujadili mapigano ya ndani Sudan
Jun 12, 2023 08:19Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) inafanya mkutano wa kilele nchini Djibouti leo Jumatatu ili kuzishawishi pande mbili katika mgogoro wa Sudan kufanya mazungumzo ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, wakati huu ambapo mji mkuu Khartoum unashuhudia mapigano makali.
-
MSF yatahadharisha: Ugonjwa wa kipindupindu unaenea kwa kasi kubwa nchini Kenya
Jun 03, 2023 10:25Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza kuwa kipindupindu kinaenea kwa kasi miongoni mwa watu waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi za wakimbizi nchini Kenya.
-
Sheikh Ali Saeed: Urithi wa Imam Khomeini unaendelea kuwatia moyo Waislamu + Video
May 31, 2023 09:02Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Ja'fari mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya amesema: Fikra za Imam Ruhullah Khomeini zinatia matumaini mema na ni nguzo ya kuwawezesha na kuwapa nguvu Waislamu duniani.
-
Reuters 'yasutwa' kudai kwamba majasusi wa China wamefanya udukuzi mkubwa dhidi ya Kenya
May 26, 2023 02:40Serikali ya Kenya imesema madai yaliyotolewa na shirika la habari la Reuters, kwamba China imekuwa ikifanya udukuzi kwa miaka mingi dhidi ya nchi hiyo ni "propganda" tu.
-
"Yesu wa Tongaren" afikishwa mahakamani nchini Kenya
May 12, 2023 08:48Raia wa Kenya aliyejitangaza kuwa ni Yesu na kuanzisha Kanisa la New Jerusalem eneo la Tongaren, Bungoma, alitarajiwa kurejeshwa mahakamani leo Ijumaa baada ya kulala kwenye seli ya polisi.
-
Mchungaji Paul Mackenzie na wenzake kubakia rumande kwa siku 30 Kenya
May 10, 2023 11:46Mhubiri tata wa Kikristo Paul Mackenzie anayekabiliwa na tuhuma za kuwashawishi wafuasi wake wafunga ili wawe wa kwanza kwenda mbinguni na kukutana na Yesu, Paul Mackenzie na mkewe Rhoda Maweu pamoja na washukiwa wengine 16 watazuiliwa kwa siku 30 gerezani.
-
Uchunguzi wa maiti katika mauaji tata ya Shakahola, Kenya waondoa uwezekano wa kuwepo uvunaji wa viungo
May 08, 2023 10:23Uchunguzi wa kidaktari uliofanyiwa miili 112 ya wahanga wa mauaji tata ya Shakahola iliyofukuliwa katika makaburi mbalimbali katika kaunti ya Kilifi katika eneo la Pwani Kenya umeondoa uwezekano juu ya uwepo wa uvunaji viungo katika miili ya wahanga hao.
-
Rais wa Kenya: Nitatumia mamlaka yangu kama Amiri Jeshi Mkuu kuzuia maandamano ya Azimio
May 01, 2023 01:49Rais William Ruto wa Kenya amesema, yuko tayari kutumia mamlaka aliyonayo kama Amiri Jeshi Mkuu kuzuia maandamano ya Muungano wa Azimio la Umoja yaliyopangwa kufanyika kesho Jumanne yakiongozwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
-
Maiti za waliofariki katika kanisa lenye misimamo mikali Kenya zakaribia 100
Apr 27, 2023 10:48Idadi ya waathirika wanaoaminika kufa na njaa kutokana na imani kali ya Kikristo nchini Kenya imeongezeka na kufikia 98 hadi kufikia leo mchana, huku familia zingine zikisubiri habari za wapendwa wao ambao ni wafuasi wa kanisa hilo na hadi sasa hawajulikani waliko.