May 31, 2023 09:02 UTC

Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Ja'fari mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya amesema: Fikra za Imam Ruhullah Khomeini zinatia matumaini mema na ni nguzo ya kuwawezesha na kuwapa nguvu Waislamu duniani.

Sheikh Ali Saeed amesema hayo katika mahojiano na ripota wa Iranpress mjini Nairobi akizungumzia athari za fikra za mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hayati Imam Ruhullah Khomeini, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kifo cha msomi na kiongozi huyo shujaa na kusema: "Maisha ya Imam Khomeini (RA) yaliupa matumaini Umma wa Kiislamu na kuupatia ujasiri zaidi."

Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Ja'fari mjini Nairobi amesisitiza kuwa, "Urithi wa kudumu wa Imam Khomeini (RA) unaendelea kuwatia moyo Waislamu katika sehemu mbalimbali za dunia.

Sheikh Ali Saeed amesema, "Kujifunza fikra za Imam Khomeini kunawapa Waislamu uwezo kwa ajili ya maendeleo, umoja na mshikamano."

Imam Khomeini (RA) aliutaja ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, umoja na kushikamana barabara na Uislamu nchini Iran kuwa ni nuru ya mwongozo kwa mataifa mengine.

Imam Ruhullah al Musawi al Khomeini (M.A) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia tarehe 14 Khordad inayosadifiana na Jumapili tarehe 4 Juni akiwa na umri wa miaka 87.

Tags