Ayatullah Khatami: Trump amejiongezea maadui kwa madai ya kubadilisha Ghuba ya Uajemi
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema: "Kwa kudai kubadili jina la Ghuba ya Uajemi, Trump amewageuza Wairani wote wakiwemo wanamapinduzi, wasiokuwa wapinduzi, wapinzani na wasiokuwa wapinzani, kuwa maadui zake, jambo ambalo ni ishara ya upumbavu wake."
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hay oleo katika hadhara ya wauumini waliohudhuria ibara ya kisiasa na kimaanawi ya Swala ya Ijumaa katika Chuo Kikuu cha Tehran na kubainisha kwamba, Trump anapaswa kujua kwamba watu wa dini walisimama kutetea thamani za Kiislamu kwa kiwango kile kile walichosimama kutetea thamani zao za kitaifa kama walivyosimama kwa miaka minane katika vita vya kujihami kutakatifuu.
Alisisitiza: "Watu hawa wa kidini hawatamruhusu Trump kufanya kosa hili tena." Wale wanaopenda nchi yao, hata nje ya nchi, waliandamana dhidi ya Trump, na kuonyesha umoja kwamba, kuna umoja wa kitaifa.
Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa wiki hii ameeleza kuwa, hata kabla ya Uislamu, ghuba hii ilikuwa Ghuba ya Uajemi, na wanahistoria wa kale wa Kigiriki na Kirumi waliandika majina ya Bahari ya Uajemi Uajemi katika historia, na katika vyanzo vya Kiarabu, waliandika maneno al-Khalij al-Faaris (Ghuba ya Uajemi) na Bahr al-Faaris (Bahari ya Uajemi).
Kadhalika Ayatullah Khatami amezungumzia misimamo ambayo majirani wa kusini mwa nchi hii wanapaswa kuchukua kuhusiana na suala hili, na kusema: "Tunataraji majirani kuingia kwenye medani hii na kumwambia Trump kwamba sisi pia hatukubaliani na makosa haya, na kwamba Ghuba hii imekuwa Ghuba ya Uajemi tangu mwanzo na itakuwa Ghuba ya Uajemi milele."