Tanzania kunufaika na uwezo wa kiteknolojia wa Iran + Video
May 06, 2025 07:15 UTC
Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika, ulifanyika kuanzia Aprili 27 hadi Mei 1, 2025 jijini Tehran kwa ushiriki wa wawakilishi kutoka nchi 38 na wajumbe 51 rasmi. Mkutano huo pia ulifanyika sambamba na maonyesho ya uwezo wa kiuchumi wa Iran yajulikanayo kama IRAN EXPO 2025.
Miongoni mwa walioshiriki katika mkutano huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe Shariff Ali Shariff. Tumepata fursa ya kuzungumza naye ambapo amebainisha baadhi ya sekta ambazo Iran inaweza kushirikiana na Tanzania ikiwemo sekta ya teknolojia.
Tags