-
Umri wa unywaji pombe Kenya wapendekezwa kuongezwa kutoka miaka 18 hadi 21
Jul 17, 2025 11:37Mamlaka ya Taifa ya Kupambana na Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya nchini Kenya (NACADA) imetetea pendekezo lake la kutaka umri wa kisheria wa kunywa pombe nchini humo uongezwe kutoka miaka 18 hadi 21, ikitaja utafiti wa kiafya, maoni ya umma na viwango vya kimataifa kama msingi wa pendekezo hilo.
-
Kadhaa wauawa katika shambulio la al-Shabaab, Garissa Kenya
Jul 14, 2025 15:12Watu wawili wameuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulio linaloshukiwa kuwa la magaidi wa al-Shabaab katika Kaunti ya Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya.
-
Baadhi ya Waislamu Kenya wapendekeza Kadhi Mkuu ajaye atoke nje ya Pwani
Jul 14, 2025 06:56Baada ya kupita siku chache tu tangu alipoaga dunia Kadhi Mkuu wa Kenye Sheikh Abdulhalim Hussein Athman, baadhi ya Waislamu wamependekeza kadhi ajaye atoke nje ya eneo la Pwani.
-
Mkuu wa Mawaziri Kenya atofautiana na Rais Ruto kuhusu kuwapiga risasi waandamanaji
Jul 14, 2025 03:13Mkuu wa Mawaziri wa Mawaziri nchini Kenya, Musalia Mudavadi ametofautiana na Rais William Ruto kuhusu wito wake wa kupigwa risasi viijana wanaoandamana kupinga sera za serikali yake na amevitaka vyombo vya usalama visiwaumize Wakenya wakati wa maandamano.
-
Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Abdulhalim aaga dunia, amezikwa leo
Jul 10, 2025 13:13Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Abdulhalim Hussein Athman amefariki dunia usiku wa manane wa kuamkia leo mjini Mombasa na maziko yake yamefanyika leo.
-
Mahakama Kenya yaiamuru polisi iache kufunga jiji la Nairobi wakati wa maandamano
Jul 10, 2025 07:04Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa amri ya kuwazuia polisi kuweka vizuizi au kuzuia raia kufika katikati mwa jiji la Nairobi wakati wa maandamano. Jaji wa mahakama hiyo Lawrence Mugambi alitoa amri hiyo jana Jumatano kufuatia kesi iliyowasilishwa na Katiba Institute baada ya jiji kufungwa wakati wa maandamano ya Saba Saba mnamo Jumatatu wiki hii.
-
Waendesha mashtaka Kenya: Waandamanaji 37 watafunguliwa mashtaka ya ugaidi
Jul 09, 2025 08:05Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itafungua mashtaka ya ugaidi dhidi ya watu 37 waliokamatwa kwenye maandamano ya kuipinga serikali mwishoni mwa mwezi Juni.
-
Umoja wa Mataifa 'washtushwa' na mauaji ya waandamanaji Kenya
Jul 08, 2025 14:20Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi mkubwa juu ya vifo vya watu zaidi ya 10 nchini Kenya, ambapo polisi na waandamanaji walikabiliana wakati wa maandamano ya kupinga sera za serikali ya nchi hiyo Jumatatu.
-
11 wauawa Kenya katika maandamano ya kumbukumbu ya vuguvugu la demokrasia
Jul 08, 2025 06:31Watu wasiopungua 11 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa wakati wa maandamano ya kuadhimisha miaka 35 ya kumbukumbu ya vuguvugu la kupigania demokrasia maarufu kama Saba Saba.
-
EACC: Wanafunzi Kenya wanatumiwa na viongozi kusajili kampuni hewa za kupora pesa
Jun 28, 2025 08:28Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ya Kenya (EACC) imefichua mpango, ambapo maafisa wa juu wa serikali za Kaunti, wakiwemo magavana wanadaiwa kuwahusisha wanafunzi walioko kwenye mafunzo ya kazi kama njia ya kufuja mabilioni ya pesa za umma kupitia kampuni hewa.