-
Mbunge 'Jaguar' anyimwa dhamana nchini Kenya + Sauti
Jun 28, 2019 12:43Mahakama nchini Kenya imemnyima dhamana, Mbunge wa eneobunge la Starehe jijini Nairobi Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ ambaye alikamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda wanaoishi katika nchini hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mbunge huyo atasalia korokoroni hadi pale kesi yake itakaposikilizwa tena. Mwandishi wetu wa Mombasa, Kenya Seifullah Murtadha ana maelezo zaidi......
-
Kamati ya Mshikamano wa Wakenya na Wapalestina: Muamala ya Karne utagonga mwamba
Jun 27, 2019 12:29Vuguvugu la mshikamano baina ya Wakenya na Wapelestina limekosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Mbunge Jaguar wa Kenya aliyetaka kutimuliwa wafanyabiashara wa kigeni atiwa mbaroni
Jun 26, 2019 08:00Mbunge wa Jimbo la Starehe jijini Nairobi nchini Kenya, Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ amekamatwa leo na jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda wanaoishi katika nchini hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
-
Mgonjwa mwenye dalili za Ebola Kenya awekwa karantini
Jun 17, 2019 08:01Mgonjwa anayeshukiwa kuwa na Ebola nchini Kenya amewekwa katika karantini katika Hospitali ya Kericho magharibi mwa nchi hiyo.
-
Al-Shabaab: Tumehusika na mashambulizi ya Kenya na Somalia yaliyoua 16
Jun 15, 2019 22:52Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab limetangaza kuwa limehusika na miripuko ya mabomu iliyoua watu 16 hapo jana Jumamosi katika nchi za Kenya na Somalia.
-
Bomu la kutegwa ardhini laua askari polisi 10 nchini Kenya + Sauti
Jun 15, 2019 08:11Maafisa usalama wasiopungua 10 wameripotiwa kuuawa baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini katika kaunti ya Wajir, katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya.
-
Wakenya waandamana jijini Nairobi kupinga mradi wa makaa ya mawe Lamu + Sauti
Jun 12, 2019 12:06Mashirika ya kijamii nchini Kenya yakiongozwa na shirika la deCOALonize la kutetea nishati safi wameandaa maandamano makubwa jijini Nairobi kupinga hatua ya serikali ya nchi hiyo kuendelea kufadhili ujenzi wa kiwanda cha kawi ya mawe kisiwani Lamu katika mpaka wa Kenya na Somalia. Omar Elmawi ni mratibu wa kitaifa wa shirika hilo la deCOALonize. Mwandishi wetu wa Mombasa Kenya Seifullah Murtadha amefanya mahojiano naye na hapa anaanza kuelezea kiini cha maandamano hayo
-
Polisi Kenya wamjeruhi vibaya kwa risasi kijana aliyetaka kuingia Ikulu kwa nguvu + Sauti
Jun 11, 2019 12:08Polisi nchini kenya wamempiga risasi na kumjeruhi vibaya jamaa mmoja aliyekua akijaribu kuingia katika ikulu ya rais jijini Nairobi huku akiwa amejihami kwa kisu mkononi. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.
-
Mkenya atakiwa aukane uraia wa Marekani kabla ya kuwa balozi
Jun 07, 2019 02:53Raia wa Kenya ambaye pia ana uraia wa Marekani ametakiwa aukane uraia wa Marekani kabla ya kuchukua nafasi ya balozi wa Kenya nchini Korea Kusini.
-
Kenya yazindua sarafu mpya Madaraka Day + Sauti
Jun 01, 2019 12:23Taifa la kenya limezindua sarafu mpya katika maadhimisho ya 56 ya Madaraka Day ili kupambana na ufisadi. Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa, pasi na kushirikiana ili kuukomesha ufisadi basi ndoto za waanzilishi wa taifa za kuona Kenya ni taifa lililostaarabika katika kila Nyanja, zitashindwa kutimia. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.