-
Mawaziri wenye misimamo mikali wa Netanyahu: Usitishaji vita wa kudumu ni sawa na kuvunjwa baraza la mawaziri
Nov 29, 2023 07:36Mawaziri wawili wenye misimamo mikali katika baraza la mawaziri la muungano wa Benjamin Netanyahu wamemtishia kwamba watashinikiza kuvunjwa baraza lake la mawaziri endapo usitishaji vita wa kudumu utafikiwa huko Gaza.
-
Makubaliano ya kusitisha vita Gaza yarefushwa kwa siku 2 zaidi
Nov 28, 2023 07:12Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar na Harakati ya Hamas zimetangaza kuwa, makubaliano ya usitishaji vita huko Gaza yameongezwa muda kwa siku mbili zaidi, kwa msingi wa masharti yale yale ya awali.
-
Amir-Abdollahian: Uungaji mkono wa Marekani kwa Israel ulisababisha kuendelea kwa vita Gaza
Nov 24, 2023 12:02Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kama si msaada na himaya ya Marekani kwa utawala ghasibu wa Israel, utawala huo bandia haungeweza kuendeleza vita na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
-
Hatimaye vita vya Gaza vyasimamishwa kwa muda wa siku 4
Nov 22, 2023 06:39Hatimaye kumefikiwa makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza kwa muda wa siku nne ili kutoa fursa ya kufikishwa misaada ya kibinadamu na pande mbili kubadilishana mateka.
-
Upinzani wa Wamagharibi kwa usitishaji vita Gaza
Nov 14, 2023 09:23Licha ya kupita karibu siku 40 tangu ilipotokea operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa na radiamali ya utawala wa Kizayuni kwa operesheni hiyo kwa kushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza na kuuawa maelfu ya Wapalestina na uharibifu mkubwa wa eneo hilo, lakini baadhi ya madola ya Magharibi yakifungamana na Waziri Mkuu wa utawala huu, Benjamin Netanyahu, bado yangali yanapinga usitishaji wa vita hivi vya umwagaji damu.
-
Netanyahu akataa ombi la Biden la kusitisha mapigano kwa siku 3 huko Gaza
Nov 09, 2023 02:18Rais Joe Biden wa Marekani amemtaka Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel asitishe mapigano kwa siku tatu ili kutatua suala la mateka. Kuhusiana na jambo hilo, Biden amesema katika mazungumzo ya simu yaliyofanyika siku ya Jumanne alimuomba Benjamin Netanyahu asitishe mapigano ili kuandaa uwanja wa kushughulikiwa suala la mateka wa Israel.
-
Misimamo inayogongana ya White House na Biden kuhusu kusitishwa mapigano huko Ghaza
Nov 03, 2023 03:27Ikiwa zimepita takribani wiki 4 tangu kuanza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na mashambulizi ya jinai ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa maelfu ya Wapalestina hususan watoto na wanawake, Marekani ambayo ni muungaji mkono mkuu na mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni, bado inataka kuendelezwa mauaji ya umwagaji damu huko Ghaza.
-
Upinzani mkali wa Marekani dhidi ya juhudi za kusitisha vita Ghaza
Oct 24, 2023 10:03Marekani ikiwa ni mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni si tu kwamba inatoa misaada ya kila aina ya silaha na fedha kwa ajili ya kuushambuliwa Ukanda wa Ghaza, bali pia inapinga vikali usitishwaji vita katika uvamizi huo wa umwagaji damu kwa visingizio vya uongo na visivyo na msingi.
-
Pande hasimu Sudan zafikia makubaliano mapya ya usitishaji vita ya saa 72
Jun 18, 2023 11:19Pande mbili zinazopigana nchini Sudan, jeshi la taifa SAF na kikosi cha uusaidizi wa haraka (RSF), zimekubaliana kusitisha mapigano kwa saa 72 kuanzia Jumapili ya leo.
-
Makubaliano ya awali ya pande zinazozozana Sudan kwa ajili ya kusitisha mapigano
May 13, 2023 07:22Hatimaye baada ya siku tatu za mazungumzo magumu ya kurudisha amani nchini Sudan, pande mbili zinazohasimiana zimetia saini taarifa na kukubaliana kuwa maslahi ya watu wa nchi hiyo yapewe kipaumbele. Pande hizo zimekubali kuchukua hatua zote za lazima ili kutowadhuru raia na kuwaruhusu waondoke kwenye maeneo yenye mapigano na yaliyozingirwa.