-
Marekani yakwamisha azimio la Baraza la Usalama kuhusu mauaji ya wahajiri Libya
Jul 04, 2019 07:32Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilimaliza kikao chake cha faragha jana jioni kwa wakati wa New York kuhusiana na Libya bila ya kuafikiana mwafaka kuhusu shambulizi la anga lililolenga makazi ya wahajiri katika eneo la Tajoura huko mashariki mwa Tripoli ambalo limeua wakimbizi 60 na kujeruhi wengine zaidi ya 130.
-
AU yalaani kushambuliwa wahajiri nchini Libya
Jul 04, 2019 02:43Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amelaani shambulio la anga lililofanywa na jenerali muasi Khalifa Haftar dhidi ya kituo cha kuhifadhia wahajiri karibu na Tripoli, mji kuu wa Libya.
-
Seneti yataka kuchunguzwa uwepo wa silaha za Marekani nchini Libya
Jul 03, 2019 12:53Mkuu wa Kamati ya Baraza la Seneti la Marekani ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu silaha za nchi hiyo zilizotumiwa na jeshi la jenerali muasi wa Libya Khalifa Haftar.
-
40 wauawa, 80 wajeruhiwa katika shambulizi la anga dhidi ya kituo cha wahajiri Libya
Jul 03, 2019 02:49Watu wasiopungua 40 wameuawa huku wengine zaidi ya 80 wakijeruhiwa katika shambulizi la anga lililolenga kituo cha kuwazuilia wahajiri haramu mashariki mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.
-
Makombora ya Marekani yanaswa Libya katika ngome ya Haftar
Jun 30, 2019 07:43Wanajeshi wa serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj na ambayo inaungwa mkono na jamii ya kimataifa wamenasa makombora ya Marekani yaliyokuwa yakitumiwa na vikosi vinavyojiita Jeshi la Kitaifa linaloongozwa na kamanda muasi Khalifa Haftar.
-
Walibya wamfungulia Khalifa Haftar mashitaka ya jinai za kivita
Jun 28, 2019 15:28Raia wa Libya wanaoishi Marekani wamemfungulia mashitaka ya jinai za kivita kamanda muasi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, Jenerali Khalifa Haftar wakisisitiza kuwa wapiganaji wa kamanda huyo wameua jamaa zao katika mashambulizi ya hivi karibuni ya mabomu katika mji mkuu Tripoli.
-
Askari wa Ufaransa na Imarati wanaswa wakishirikiana na Haftar, Libya
Jun 28, 2019 07:43Askari wa Ufaransa na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) wamekuwa wakishirikiana na wapiganaji wa kundi la Jenerali Khalifa Haftar linalopiganaji dhidi ya serikali inayotambuliwa rasmi kimataifa ya Libya.
-
Baada ya kupata pigo, hatimaye Jenerali Khalifa Haftar alazimika kukubali mazungumzo Libya
Jun 27, 2019 11:05Wapiganaji wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya wamelazimika kukubali mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo ulioanzishwa na kundi hilo linaloungwa mkono na Saudi Arabia, Imarati, Misri na Ufaransa.
-
Jitihada za serikali ya Muafaka wa Kitaifa Libya za kukomesha mgogoro wa ndani
Jun 18, 2019 02:24Kutokana na kuendelea mgogoro na vita vya ndani nchini Libya na hali mbaya inayotawala nchini humo, kiongozi wa serikali ya Muafaka wa Kitaifa ametoa wito wa kuundwa Jukwaa la Libya kwa shabaha ya kutatua mgogoro wa nchi hiyo na kuunda baraza la mapatano ya kitaifa.
-
Fayez al-Sarraj ataka uchaguzi ufanyike Libya kabla ya kumalizika mwaka
Jun 17, 2019 07:49Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ametoa mwito wa kufanyika uchaguzi nchini humo kabla ya mwisho wa mwaka huu. Awali uchaguzi mkuu nchini humo ulikuwa umepangwa kufanyika Disemba 10 mwaka jana 2018 lakini zoezi hilo liliahirishwa kutokana mpasuko uliojitokeza baina ya viongozi wa mirengo hasimu ya kisiasa na wimbi la mapigano na machafuko yaliyozuka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.