-
Makumi ya maiti zagunduliwa katika kaburi la umati Sirte, Libya
Oct 03, 2022 07:43Mamlaka ya Libya imetangaza kupatikana kwa miili 42 ambayo haikutambuliwa katika kaburi la pamoja huko Sirte, makao makuu ya zamani ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).
-
Kikao cha kimataifa cha Berlin kuhusu Libya na suala zima la uchaguzi mkuu
Sep 11, 2022 09:22Nchi zilizoshiriki katika katika kikao cha kimataifa cha Berlin kuhusu Libya zimesisitiza kuwa, uchaguzi ndiyo njia pekee ya utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo. Kikao hicho cha siku mbili kimehudhuriwa pia na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Uingereza, Marekani, Uturuki, Italia, Ujerumani na Misri.
-
Umoja wa Mataifa: Hakuna suluhisho la kijeshi la mzozo wa Libya
Sep 08, 2022 02:50Msaidizi wa Katibu Mkuu na Mratibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amesisitiza kuwa, hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo wa nchi hiyo, na kwa mara nyingine ametoa wito wa kufanyika uchaguzi nchini Libya haraka iwezekanavyo.
-
UN yawahamishia Rwanda watafuta hifadhi 100 kutoka Libya
Sep 02, 2022 12:06Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limetangaza kuwa limewahamishia nchini Rwanda makumi ya watu wanaotafuta hifadhi waliokuwa nchini Libya.
-
Hofu ya UN juu ya mgogoro wa kisiasa nchini Libya
Aug 31, 2022 07:12Mkuu wa Siasa wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa, kutotatuliwa mgogoro wa kisiasa wa Libya na kutofanyika uchaguzi uliocheleweshwa ni tishio kwa hali ya mambo katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Kushadidi mgogoro nchini Libya kwa kuanza tena vita na mapigano makali
Aug 29, 2022 13:11Kufuatia kushadidi mzozo wa kisiasa nchini Libya kati ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Abdul Hamid al-Dbeibeh na serikali mpya iliyopewa mamlaka na Bunge inayoongozwa na Fathi Bashagha, mapigano yameanza upya kati ya vikosi vya pande hizo mbili katika mji mkuu Tripoli.
-
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yasikitishwa na machafuko mapya ya Libya
Aug 28, 2022 10:42Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran ameelezea kusikitishwa sana na machafuko mapya ya nchini Libya na ametaka kukomeshwa mara moja mapigano hayo. Amesema, Tehran inazitaka pande hasimu kuzingatia maslahi ya taifa, usalama wa wananchi na kutatua mambo yao kwa njia ya mazungumzo.
-
Watu 23 wauawa na kadhaa wajeruhiwa baada ya mapigano kuzuka upya katika mji mkuu wa Libya
Aug 28, 2022 03:55Duru za tiba nchini Libya zimeripoti kuwa watu wasiopungua 23 wameuawa na kwa uchache 87 wamejeruhiwa katika mapigano makali yaliyozuka upya Jumamosi asubuhi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.
-
Maiti 20 za wahajiri zapatikana katika mpaka wa Libya na Sudan
Aug 13, 2022 11:24Maiti 20 za wahajiri haramu zimepatikana katika jangwa lililoko baina ya Libya na Sudan.
-
Watu kadhaa wauawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama vya Libya mjini Tripoli
Jul 22, 2022 11:57Mapigano makali yaliyozuka kati ya makundi yanayohasimiana katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, yamesababisha vifo vya watu kadhaa huku kukiwa na wasiwasi kwamba huenda mzozo wa kisiasa ukazusha upya nchini humo.