-
Watunisia waandamana kupinga mageuzi ya kijamii yaliyopendekezwa na kamati ya Rais
Aug 12, 2018 03:24Maelfu ya wananchi wa Tunisia wameandamana kupinga mageuzi ya kijamii yaliyopendekezwa na kamati iliyoundwa na rais wa nchi hiyo Beji Caid Essebsi.
-
Hamas yataka kuendeleza maandamano ya Kurejea
Aug 10, 2018 11:49Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas amesisitiza kuwa wananchi wa Palestina wataendelea kufanya maandamano makubwa ya "Haki ya Kurejea" hadi pale malengo yao yatakapofanikishwa na kuvunjwa mzingiro wa Ghaza.
-
Wananchi wa Libya waandamana kulalamikia maisha magumu
Aug 05, 2018 10:48Miji mingi ya Libya imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia maisha magumu.
-
Wananchi wa Bahrain wafanya maandamano makubwa kuonyesha mshikamano wao kwa maulamaa walioko jela
Jul 31, 2018 02:19Wananchi wa Bahrain jana usiku walifanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini humo lengo likiwa ni kuwaunga mkono na kuonyesha mshikamano wao kwa maulamaa na wanazuoni wa kidini wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala wa Aal Khalifa.
-
Utawala wa Kizayuni wazidisha idadi ya wanajeshi wake katika mipaka ya Ukanda wa Ghaza
Jul 26, 2018 23:33Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel imeongeza idadi ya wanajeshi wake katika mipaka ya Ukanda wa Ghaza kwa kuhofia maandamano ya raia wa Palestina katika Ijumaa ya 18 yajulikanayo kwa jina la "Haki ya Kurejea ambayo yanatazamiwa kufanyika leo katika maeneo ya mpaka wa Ghaza na Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Raia wazalendo wa Marekani waandamana dhidi ya siasa za Donald Trump
Jul 22, 2018 23:29Raia asili wa Marekani na wasio wazungu, wamefanya maandamano kupinga siasa mbovu za hali ya hewa zinazotekelezwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo.
-
Maelfu waandamana Tel Aviv kupinga ubaguzi wa Israel
Jul 15, 2018 02:51Watu zaidi ya elfu saba wamefanya maandamano katika barabara za mji wa Tel Aviv kupinga muswada wa kibaguzi wa utawala haramu wa Israel.
-
Maandamano makubwa ya wananchi wa Uingereza wakipinga safari ya Trump mjini London
Jul 13, 2018 10:53Wimbi kubwa la wananchi wa Uingereza limefanya maandamano makubwa kupinga ziara ya Rais wa Marekani mjini London. Maandamano hayo yamefanyika kufuatia wito uliotolewa na taasisi za kutetea haki za binadamu na harakati zinazopinga vita za nchini humo.
-
Maandamano dhidi ya chama tawala yafanyika Zimbabwe
Jul 11, 2018 23:41Maelfu ya wafuasi wa upinzani jana Jumatano walijitokeza mabarabarani kushiriki maandamano dhidi ya chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-pf katika mji mkuu Harare.
-
Polisi yatumia mabomu kuzima maandamano Uganda
Jul 11, 2018 09:07Maafisa wa polisi nchini Uganda wametumia mabomu ya kutoa machozi kuzima maandamano ya wananchi waliomiminika katika barabara za mji mkuu Kampala, kulalamikia kodi mpya wanazotozwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.