Raia wazalendo wa Marekani waandamana dhidi ya siasa za Donald Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46952-raia_wazalendo_wa_marekani_waandamana_dhidi_ya_siasa_za_donald_trump
Raia asili wa Marekani na wasio wazungu, wamefanya maandamano kupinga siasa mbovu za hali ya hewa zinazotekelezwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 22, 2018 23:29 UTC
  • Raia wazalendo wa Marekani waandamana dhidi ya siasa za Donald Trump

Raia asili wa Marekani na wasio wazungu, wamefanya maandamano kupinga siasa mbovu za hali ya hewa zinazotekelezwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Maandamano hayo ya kupinga siasa mbovu za hali ya hewa zinazotekelezwa na Trump yamefanyika katika mitaa kadhaa ya jiji la Washington, D.C. Aidha maandamano hayo yameitishwa na Shirika la 'Zero Hour' ambapo washiriki walibeba mabango yenye jumbe ambazo zinalaani siasa za rais huyo wa Marekani na kuzitaja kuwa ndizo chanzo cha mabadiliko ya tabianchi.

Rais Donald Trump alipoiondoa nchi yake katika mkataba wa kimataifa wa hali ya hewa

Itakumbukwa kwamba mwaka jana, Rais Donald Trump aliiondoa nchi yake katika mkataba wa hali ya hewa wa mjini Paris, Ufaransa hatua ambayo ilikabiliwa na radiamali hasi kutoka pembe tofauti za dunia. Kwa kuzingatia kuwa Marekani ndio mzalishaji mkubwa wa gesi inayotokana na viwanda katika ngazi ya kimataifa, inahesabika kuwa mchafuzi mkuu wa mazingira duniani.