Watunisia waandamana kupinga mageuzi ya kijamii yaliyopendekezwa na kamati ya Rais
Maelfu ya wananchi wa Tunisia wameandamana kupinga mageuzi ya kijamii yaliyopendekezwa na kamati iliyoundwa na rais wa nchi hiyo Beji Caid Essebsi.
Wananchi hao wanaojumuisha watu wa matabaka mbalimbali wakiwemo wasomi wa vyuo vikuu na shakhsia wa dini ya Kiislamu wameandamana kuitikia wito uliotolewa na jopo la "Uratibu wa Kitaifa kwa ajili ya Kulinda Qur'ani na Katiba" na kutangaza upinzani wao dhidi ya mapendekezo hayo ya mageuzi ya kijamii.
Huku wakiwa na misahafu mikononi mwao, waandamanaji hao wamesisitiza kuwa wataulinda na kuuhami Uislamu kwa damu zao.
Kutokana na kampeni ya uhuru wa mtu binafsi inayoendeshwa nchini Tunisia, kamati iliyoundwa na rais wa nchi hiyo mwaka uliopita wa 2017 iliwasilisha mapendekezo makubwa ya kijamii ambayo hayajawahi kushuhudiwa yakiwemo ya kutaka mirathi itolewe kwa usawa kati ya mwanamke na mwanamme, kuondolewa hukumu ya kuwa kosa la jinai maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja na vile vile kufutwa hukumu ya adhabu ya kifo.../