Maelfu waandamana Tel Aviv kupinga ubaguzi wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46791-maelfu_waandamana_tel_aviv_kupinga_ubaguzi_wa_israel
Watu zaidi ya elfu saba wamefanya maandamano katika barabara za mji wa Tel Aviv kupinga muswada wa kibaguzi wa utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2018 02:51 UTC
  • Maelfu waandamana Tel Aviv kupinga ubaguzi wa Israel

Watu zaidi ya elfu saba wamefanya maandamano katika barabara za mji wa Tel Aviv kupinga muswada wa kibaguzi wa utawala haramu wa Israel.

Waandamanaji hao wakiwemo wanasiasa, wanaharakati wa kijamii na wabunge Waisraeli walifanya maandamano haya jana Jumamosi kuonesha upinzani wao kwa muswada wa sheria inayotaka kutambuliwa Israel kama 'dola la Mayahudi pekee'.

Muswada huo unatazamiwa kupigiwa kura katika kikao cha kesho cha bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel (Knesset).

Muswada huo unazifadhilisha 'thamani za Kizayuni' badala ya 'thamani za kidemokrasia' katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Waandamanaji mjini Tel Aviv wakiwa na mabango

Aidha muswada huo unautambua Quds kama mji mkuu wa Israel, kutaka kutambuliwa jamii ya Wayahudi pekee katika ardhi hizo za Palestina, sanjari na kukitambua Kiebrania kama lugha rasmi na kukitweza Kiarabu.

Taarifa ya waandaaji wa maandamano ya jana mjini Tel Aviv inasema, "Sheria hiyo iwapo itapasishwa, itaufanya ubaguzi, ujamii na utengano kama sehemu ya kila siku ya maisha yetu."