-
Mafuriko yaua makumi ya watu Afghanistan, 150 hawajulikani waliko
Jul 30, 2021 12:35Makumi ya watu wamepoteza maisha huku wengine wengi wakitoweka kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba Afghanistan.
-
Idadi ya watu waliofariki katika mafuriko yaliyotokea Ulaya imefika 153
Jul 17, 2021 07:49Watu 153 wamefariki dunia hadi sasa kutokana na mafuriko yaliyotokana na mvua kali zilizonyesha magharibi na kaskazini mwa Ulaya na kusababisha mito kufurika na kingo zake kupasuka.
-
Makumi wafariki dunia kutokana na mafuriko, maporomoko ya ardhi Indonesia
Apr 04, 2021 12:50Makumi ya watu wamepoteza maisha na wengine wengi hawajulikani walipo baada ya kutokea mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Indonesia.
-
UN: Mafuriko yameua watu 35 nchini Somalia, milioni 1.6 wameathiriwa
Oct 29, 2020 07:06Umoja wa Mataifa umetangaza habari ya kupoteza maisha watu 35 nchini Somalia kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha nchini humo.
-
Majanga ya kimaumbile yaongezeka maradufu duniani kote
Oct 13, 2020 12:09Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa majanga ya kimaumbile yameongezeka maradufu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita huku mabadiliko ya tabianchi yakitajwa kuwa sababu kuu ya hali hiyo.
-
Watu milioni moja waathiriwa na mafuriko nchini Ethiopia
Oct 01, 2020 07:50Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa watu milioni moja wameathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha nchini Ethiopia, ambapo laki tatu miongoni mwao wamelazimika kuyahama makazi yao.
-
Hasara za mafuriko zaongezeka nchini Sudan
Sep 19, 2020 07:32Idara ya Ulinzi wa Raia nchini Sudan imetangaza habari ya kuongezeka hasara za roho za watu na mali kutokana na mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo. Kwa mujibu wa idara hiyo, zaidi ya watu laki saba na 70 elfu wamepata hasara kutokana na mafutiko hayo.
-
Mafuriko yaua watu zaidi ya 70 nchini Nigeria
Sep 18, 2020 08:06Kwa akali watu 77 wameaga dunia kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha nchini Nigeria.
-
Mvua na mafuriko yaua na kujeruhi makumi nchini Burkina Faso
Sep 10, 2020 15:51Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa nchi hiyo inakabiliwa na janga la kimaumbile baada ya watu 13 kupoteza maisha kutokana na mafuriko, huku wengine 19 wakijeruhiwa.
-
Sudan yaomba msaada wa kimataifa kwa waathiriwa wa mafuriko
Sep 08, 2020 16:22Waziri wa Afya wa Sudan ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kujitokea maradhi ya kuambukiza katika siku kadhaa zijazo kutokana na maafa yaliyosababisha na mafuriko makubwa yanayoendelea nchini humo.