-
Rais Rouhani: Serikali itafidia hasara walizopata waathiriwa wa mafuriko
Mar 27, 2019 16:10Rais Hassan Rouhani amesema: Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu itahakikisha kwa suhula zote ilizonazo na kwa uwezo wake wote inafidia hasara walizopata watu wote walioathiriwa na mafuriko.
-
Kiongozi Muadhamu atoa ujumbe na kutaka kusaidiwa haraka waathiriwa wa mafuriko ya Shiraz
Mar 26, 2019 15:12Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemtumia ujumbe Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa mji wa Shiraz wa kusini mwa Iran ambapo sambamba na kutoa mkono wa pole na salamu za rambirambi kwa wananchi waliopatwa na msiba, ametoa wito kuongezwa kasi katika shughuli ya ufikishaji misaada kwa waathiriwa wa janga hilo.
-
Rais Rouhani ataka kushughulikiwa haraka hali ya waathiriwa wa mafuriko Iran
Mar 26, 2019 15:10Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza kushughulikiwa haraka hali ya wananchi waliokumbwa na janga la mafuriko katika maeneo mbalimbali hapa nchini amesema kuwa, asasi zote zinapaswa kufanya juhudi maradufu kwa ajili ya kuhakikisha wananchi hao wanafikiwa na misaada haraka iwezekanavyo.
-
Mataifa mbalimbali yatuma salamu za pole na rambirambi kufuatia janga la mafuriko Iran
Mar 26, 2019 03:08Kufuatia mafuriko yaliyoikumba mikoa kadhaa ya Iran na kupelekea kwa akali watu 19 kufariki dunia na makumi ya wengine kujeruhiwa, balozi za nchi mbalimbali hapa Tehran zimetoa mkono wa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao walioaga dunia katika maafa haya ya mafuriko.
-
Watu 17 wafariki dunia kwa mafuriko katika mkoa wa Fars, Iran
Mar 25, 2019 14:37Kwa akali watu 17 wamefariki dunia katika mkoa wa Fars wa kusini magharibi mwa Iran na makumi ya wengine wamejeruhiwa kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
-
Kutokana na kuendelea kunyesha mvua nchini Iran, Rais Rouhani amewataka wakuu wa mikoa kuwa katika hali ya tahadhari
Mar 25, 2019 13:35Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa amri kwa wakuu wote wa mikoa humu nchini kuwa katika hali ya tahadhari kutokana na mvua kuendelea kunyesha katika maeneo tofauti ya Iran.
-
Njaa inazidi kuhatarisha maisha ya watu nchini Kenya, zaidi ya milioni moja wako hatarini
Mar 24, 2019 15:37Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti leo kuwa, zaidi ya watu milioni moja wako katika hatari ya kuteketea kwa njaa katika kaunti na wilaya nyingi nchini Kenya kutokana na ukame wa muda mrefu.
-
Kiongozi Muadhamu asisitiza kusaidiwa haraka watu walioathiriwa na mafuriko kaskazini mwa Iran
Mar 23, 2019 16:28Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa tukio la mafuriko yaliyoikumba miji ya Golestan na Mazandaran kaskazini mwa Iran na kusisitiza juu ya kusaidiwa watu walioathiriwa na janga hilo la kimaumbile.
-
Mafuriko yaendelea kuua katika nchi za kusini mwa Afrika
Mar 15, 2019 01:18Makumi ya watu wamepoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Malawi.
-
Mafuriko yaua watu 45 Afghanistan na Pakistan
Mar 06, 2019 02:46Kwa akali watu 45 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika nchi za Afghanistan na Pakistan.