-
Mafuriko Jordan yauwa watu wasiopungua 18, wengi wao ni watoto
Oct 26, 2018 07:56Watu wasiopungua 18 wengi wao wakiwa ni watoto wa shule na walimu wameaga dunia katika mafuriko ya ghafla wakati walipokuwa katika matembezi ya kishule karibu na Bahari ya Chumvi (Dead Sea) nchini Jordan. Mafuriko hayo yametajwa kuwa ni maafa makubwa zaidi kuwahi kuikumba Jordan katika miaka ya karibuni.
-
Watu 100 wauawa na mafuriko nchini Nigeria
Sep 18, 2018 07:13Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Nigeria yameua watu zaidi ya 100 katika majimbo 10 ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Watu 22 wapoteza maisha na maelfu wakosa makazi kutokana na mafuriko Niger
Aug 10, 2018 03:55Waziri mmoja wa Niger amesema kuwa, watu wasiopungua 22 wamefariki dunia na maelfu ya wengine wamepoteza makazi yao kutokana na mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Waliopoteza maisha katika mafuriko, maporomoko Japan ni zaidi ya watu 140
Jul 10, 2018 07:43Watu zaidi ya 140 wamepoteza maisha, huku hatima ya makumi ya wengine ikiwa haijulikani kutokana na athari za mvua kubwa zilizonyesha magharibi na katikati mwa Japan.
-
Amisom yawanusuru watu elfu 10 kutokana na mafuriko Somalia
May 02, 2018 14:45Askari wa Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia Amisom wamehamisha na kuwapeleka nyanda za juu, raia elfu kumi wa Somalia, ambao nusra waghariki kutokana na mafuriko katika mji wa Beledweyne, ulioko yapata kilomita 335 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu.
-
Waliofariki dunia kwa kimbunga, mafuriko Vietnam wapindukia 70
Oct 16, 2017 08:07Watu wasiopungua 72 wamepoteza maisha kufikia sasa kutokana na mafuriko na vimbunga katika maeneo ya kaskazini na katikati ya Vietnam.
-
Mafuriko yaua watu 10 Kongo DR, 90 watoweka
Sep 20, 2017 13:50Watu wasiopungua 10 wamepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko mashariki mwa Jamhuri mwa Kidemokrasia ya Kongo.
-
Mafuriko yameua watu 50 nchini Niger na kuacha maelfu bila makazi
Sep 15, 2017 04:12Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kwa akali watu 50 wamefariki dunia nchini Niger kufuatia maafa ya mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Watu milioni 24 waathiriwa na mafuriko Asia ya Kusini
Aug 22, 2017 15:29Watu zaidi ya milioni 24 wameathiriwa na mafuriko makubwa kuwahi kulikumba eneo la Asia ya Kusini katika miongo kadhaa iliyopita, huku maeneo mengi ya ardhi yakiwa yameghiriki majini. Hayo yameelezwa leo na Shirika la Msalaba Mwekundu.
-
Idadi ya waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo Sierra Leone yafikia watu 500
Aug 21, 2017 03:28Maafisa wa serikali ya Sierra Leone wamesema kuwa idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko yaliyotokea Jumatatu iliyopita nchini humo imekaribia 500.