Watu 22 wapoteza maisha na maelfu wakosa makazi kutokana na mafuriko Niger
(last modified Fri, 10 Aug 2018 03:55:06 GMT )
Aug 10, 2018 03:55 UTC
  • Watu 22 wapoteza maisha na maelfu wakosa makazi kutokana na mafuriko Niger

Waziri mmoja wa Niger amesema kuwa, watu wasiopungua 22 wamefariki dunia na maelfu ya wengine wamepoteza makazi yao kutokana na mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Laouan Magadji, waziri wa masuala ya kibinadamu wa serikali ya Niger amesema kuwa, mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo tangu tarehe 6 Agosti yamewaweka kwenye hali nguvu na ya hatari zaidi ya watu elfu sita.

Amesema, mafuriko hayo yameharibu zaidi ya nyumba elfu tatu na zaidi ya eka elfu nne za kilimo, na kusomba idadi kubwa ya mifugo na vyanzo vya maji safi ya kunywa.

UN: Niger ilikumbwa na mafuriko mengi mwaka 2017

 

Waziri huyo wa serikali ya Niger ameongeza kuwa, maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ndiyo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo ambapo zaidi ya watu elfu mbili wamepoteza makazi yao huko Niamey pekee.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Niger imekumbwa na mafuriko mengi katika miaka ya hivi karibuni hasa maeneo ya jangwani ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Takwimu zilizotolewa na umoja huo zinaonesha kuwa, mwaka 2017 watu 56 wakiwemo 20 kutoka mji mkuu Niamey walipoteza maisha na laki mbili na sita wengine walipata hasara zilizosababishwa na mafuriko.

Tags