Kiongozi Muadhamu asisitiza kusaidiwa haraka watu walioathiriwa na mafuriko kaskazini mwa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i52356
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa tukio la mafuriko yaliyoikumba miji ya Golestan na Mazandaran kaskazini mwa Iran na kusisitiza juu ya kusaidiwa watu walioathiriwa na janga hilo la kimaumbile.
(last modified 2025-07-17T10:20:57+00:00 )
Mar 23, 2019 16:28 UTC
  • Kiongozi Muadhamu asisitiza kusaidiwa haraka watu walioathiriwa na mafuriko kaskazini mwa Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa tukio la mafuriko yaliyoikumba miji ya Golestan na Mazandaran kaskazini mwa Iran na kusisitiza juu ya kusaidiwa watu walioathiriwa na janga hilo la kimaumbile.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika ujumbe wake huo  ambapo sambamba na kuonyesha kusikitishwa kwake na hasara iliyosababishwa na mafuriko hayo katika miji ya Golestan na Mazandaran amebainisha kuwa, misaada ya wananchi na kuingia vyombo vya umma katika shughuli za kutoa misaada na kufidia hasara ni jukumu muhimu ambalo linaweza kupunguza sehemu ya machungu ya wananchi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matatizo yaliyotokana na mafuriko katika mkoa wa Khozestan kusini mwa Iran na kusema kuwa, watu wote wana jukumu la kuchukua hatua za haraka za kuwasiadia wananchi waliokumbwa na mafurikko katika miji mbalimbali hapa nchini.

Mafuriko ya Golestan, Iran

Wakati huo huo, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameagiza kutumiwa suhula zote kwa ajili ya kutatua matatizo yaliyosababishwa na mafuriko huko Golestan sambamba na kuandaliwa mazingira mwafaka ya kupatiwa wananchi waliothiriwa na mafuriko mahitaji ya lazima katika maeneo hayo.

Mvua kubwa ilionyesha katika mikoa ya kaskazini mwa Iran ya Golestan na Mazandaran imepelekea kutokea mafuriko makubwa ambayo yamesababisha hasara kwa wakazi wa maeneo hayo. Abdolreza Rahmani Fazli, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa serikali ameyatembelea maeneo yaliyokumbwa na mafuriko na kusema kuwa, serikali kwa kushirikiana na wananchi inafanya kila iwezalo kufidia haraka iwezekanavyo hasara iliyosababishwa na mafuriko hayo.