Pars Today
Mjumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wabunge wanaandaa hoja ya dharura wa kujadiliwa haraka na nje ya utaratibu wa kawaida wa kuanzisha tena shughuli za nyuklia kwa lengo la kukabiliana na hatua dhidi ya Iran iliyochukuliwa na Kongresi ya Marekani.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika mazingira ya hivi sasa katika Mashariki ya Kati kuna baadhi ya nchi ambazo mbali na kufanya uadui zinafanya kila ziwezalo kuzusha mifarakano katika eneo hili.
Balozi wa Palestina nchini Iran amesema kuwa Intifadha ya wananchi wa Palestina itaendelea hadi kukombolewa Quds Tukufu.
Dakta Ali Larijani amechaguliwa kuwa Spika wa bunge la kumi la Iran yaani Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu kwa kupigiwa kura na wabunge leo Jumanne.
Awamu ya 10 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, imezidnuliwa rasmi leo mjini Tehran kwa Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini.
Duru ya kumi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran imeanza rasmi leo Jumamosi katika sherehe iliyoambatana na ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Wabunge nchini Iran wamepitisha muswada wa sheria ya kuishurutisha serikali ya Iran kuitaka Marekani iilipe fidia Jamhuri ya Kiislamu kutokana na jinai za Washignton dhidi ya nchi hii na raia wake.
Kampeni za duru ya pili ya uchaguzi wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran itakayofanyika Aprili 29, zimeanza rasmi hii leo Alkhamisi.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Iran amesema kuwa maandalizi na taratibu zote za uchaguzi wa kumi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na wa tano Baraza la Wataalamu zimekamilika.
Muda wa kampeni za uchaguzi wa Bunge na Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Iran umemalizika mapema leo saa mbili asubuhi tarehe 25 Februari na wananchi wa Iran kesho Ijumaa wataelekea kwenye masanduku ya kupigia kuwachagua wawakilishi wao katika zoezi litakaloanza asubuhi na kuendelea kwa masaa kumi.