Ali Larijani awa Spika wa Majlisi ya Kumi ya Ushauri ya Kiislamu
Dakta Ali Larijani amechaguliwa kuwa Spika wa bunge la kumi la Iran yaani Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu kwa kupigiwa kura na wabunge leo Jumanne.
Uchaguzi wa kamati kuu ya bunge katika ya Majlisi ya Kumi ya Ushauri ya Kiislamu umefanyika mapema leo asubuhi na Ali Larijani amechaguliwa kuwa Spika kwa bunge hilo kwa kura za ndio 237 kati ya 276 zilizopigwa.
Ali Mutahari, Masoud Pezeshkian, Hamid Reza Haji-Babai na Muhammd Deheqan pia wote hao waligombea kiti cha Naibu Spika ambapo Masoud Pezeshkian amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Kwanza na Ali Mutahhari amekuwa Naibu Spika wa Pili.
Katika kikao cha wazi kilichofanyika Jumapili ya juzi, Ali Larijani alichaguliwa kuwa Spika wa Muda wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu. Spika wa kudumu wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran yaani Bunge amechaguliwa kwa muda wa mwaka mmoja , baada kupasishwa uchaguzi wa wabunge wa bunge hilo, bungeni.