Bunge la 10 la Iran lazinduliwa rasmi
Awamu ya 10 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, imezidnuliwa rasmi leo mjini Tehran kwa Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini.
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge hilo ilifanyika Februari 26 na duri ya Aprili 29 ambapo wabunge 290 wanaowakilisha majimbo 207 wamefanikiwa kuingia bungeni.. Wabunge hao wameanza kutekeleza majukumu yao leo baada ya kula kiapo na wanatazamiwa kuendelea hadi tarehe 27 Mei 2020.
Bunge la Iran pia linajumuisha viti maalumu vya wawakilishi wa jamii za walio wachache wakiwemo Waislamu wa madhehebu ya Sunni, Mayahudi na Wakristo.
Kati ya waliohudhuria kikao cha ufunguzi wa bunge leo ni Rais Hassan Rouhani, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama Ayatollah Sadeq Amoli Larijani na Spika wa Bunge lililopita Ali Larijani.
Kikao rasmi cha bunge kinatazamiwa kuanza kesho ambapo mchakato wa kumchagua spika unatazamiwa kuanza.