-
Makumi wauawa Sudan Kusini licha ya makubaliano ya amani
Dec 19, 2019 02:33Zaidi ya watu 100 wameuawa katika mapigano ya kikabila ndani ya mwezi mmoja uliopita nchini Sudan Kusini, licha ya pande mbili hasimu za kisiasa kukubaliana juu ya kuundwa serikali ya umoja kitaifa.
-
Watu 18 wauawa katika mapigano baina ya vikosi vya Haftar na serikali, Libya
Sep 22, 2019 03:01Kwa akali watu 18 wameuawa katika makabiliano makali baina ya vikosi vinavyojiita Jeshi la Taifa la Libya vinavyoongozwa na Jenerali mstaafu Khalifa Haftar na vile vya serikali ya mwafaka wa kitaifa kusini mwa mji mkuu, Tripoli.
-
Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa Libya yafichua: Kikosi cha jeshi la Ufaransa kinamsaidia Haftar
Aug 23, 2019 02:31Maafisa wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya wamefichua kuwa kundi moja la jeshi la Ufaransa linalomsaidia jenerali mstaafu Khalifa Haftar limewajengea wapiganaji wa kiongozi huyo muasi kituo cha kurushia ndege zisizo na rubani katika bandari ya mafuta ya al Sidr huko kaskazini mwa Libya.
-
UNHCR: Zaidi ya watu laki 3 wamekimbia mapigano Kongo DR
Jun 18, 2019 12:35Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema zaidi ya watu laki tatu wameikimbia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kutokana na mapigano ya kikabila.
-
Kuendelea mapigano nchini Libya; tishio kwa usalama wa kimataifa
May 14, 2019 11:52Sambamba na kuendelea mapigano nchini Libya na kupanuka wigo wake, Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya wametoa taarifa iliyoyataja mashambulio ya jeshi la taifa la Libya dhidi ya mji mkuu Tripoli na viunga vyake kwamba ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.
-
Mapigano katika mji ulioathiriwa na Ebola DRC yaua watu 9
May 08, 2019 13:45Kwa akali watu tisa wameripotiwa kupoteza maisha katika mapigano baina ya askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wanamgambo waliobeba silaha katika mji wa Butembo ulioathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola.
-
Libya katika kinamasi cha mapigano ya ndani na uingiliaji wa madola ajnabi
Apr 24, 2019 06:28Mapigano nchini Libya hasa katika mji wa Tripoli na pambizoni mwake yanakuwa makali siku baada ya siku. Duru za kijeshi za Serikali ya Umoja wa Kitaifa zimetangaza kuwa, vikosi vyake vimefanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya uwanja wa ndege wa Tripoli. Hata hivyo wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar wamedai kuwa wamekaribia mno kuingia katikati ya Tripoli.
-
WHO: Idadi ya waliouawa katika mapigano ya Tripoli, Libya yapindukia watu 200
Apr 18, 2019 13:25Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa, idadi ya watu waliopoteza maisha katika mashambulizi ya vikosi vya Jenerali Khalifa Haftar vya kutaka kuudhibiti mji mkuu wa Libya, Tripoli imeongezeka na kufikia watu 205.
-
UN: Watu 56 wameuawa katika mapigano yanayoendelea Libya
Apr 11, 2019 13:58Umoja wa Mataifa umesema mapigano kati ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa na vile vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya yamesababisha watu 56 kupoteza maisha kufikia sasa.
-
Kongamano la 'amani na uchaguzi' Libya laakhirishwa kutokana na mapigano
Apr 10, 2019 07:46Mkutano wa kujadili mgogoro wa Libya na maandalizi ya uchaguzi ujao nchini humo uliotazamiwa kufanyika kati ya Aprili 14 na 16 magharibi mwa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta umeakhirishwa kutokana na kushadidi mapigano kati ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa na vile vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.