-
Maelfu ya watoto wahajiri wanashikiliwa katika mazingira ya kuogofya Marekani
May 28, 2021 07:49Watoto zaidi ya 4,300 ambao hawana wazazi wala wasimamizi na ambao waliingia nchini Marekani wakitokea Mexico wanazuiliwa katika mazingira ya kutisha jimboni Texas.
-
Biden ataka Congress ichukue hatua baada ya watu wengine 8 kuuawa kwa risasi Marekani
May 27, 2021 03:44Rais Joe Biden wa Marekani amelitaka Bunge la Kongresi la nchi hiyo litekeleze hatua za kukomesha janga la uhalifu wa silaha za moto nchini humo, masaa machache baada ya Wamarekani wanane kuuawa katika tukio jingine la ufyatuaji risasi.
-
Umoja wa Ulaya wakaribisha kurefushwa makubaliano ya kiufundi kati ya Iran na IAEA
May 26, 2021 03:59Enrique Mora Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya Kuhusu Hatua za Kigeni amekaribisha makubaliano ya kiufundi yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA na kuyataja kuwa 'makuabaliano mazuri.' Amesema makubaliano hayo yataandaa uwanja unaofaa kwa ajili ya kufikiwa mapatano ya kuridhisha mjini Vienna.
-
Vijana wengi Wakristo Marekani wachukizwa na jinai za utawala wa Kizayuni
May 26, 2021 02:40Uchunguzi mpya wa maoni unaonesha kuwa, uungaji mkono wa vijana wengi Wakristo nchini Marekani umepungua kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya watoto na watu wasio na hatia huko Palestina.
-
Ufaransa yakiri kuhusu utambulisho wa kigaidi wa utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina
May 25, 2021 06:03Jumapili iliyopita Jean-Yves Le Drian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa aliashiria hujuma ya kinyama iliyofanywa karibuni na utawala haramu wa Israel katika miji kadhaa ya Waarabu katika ardhi unazozikalia kwa mabavu na kutahadharisha dhidi ya ubaguzi wa rangi unaotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina.
-
Kufika ukingoni subira ya makundi ya muqawama ya Iraq kuhusu wanajeshi wa Marekani
May 24, 2021 21:47Kituo cha Uratibu wa Makundi ya Muqawama ya Iraq kimetoa taarifa kikisema muhula waliokuwa wamepewa askari vamizi wa Marekani kuondoka Iraq umefika ukingoni na sambamba na hilo kumeshadidishwa oparesheni dhidi ya maeneo waliko magaidi hao wa Marekani nchini Iraq.
-
Axios: Marekani ilikuwa na taarifa kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina
May 23, 2021 22:02Tovuti ya habari ya Kimarekani ya Axios imeripoti kuwa, serikali ya Washington ilikuwa na taarifa kitambo nyuma kabla ya kuanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Wapalestina tarehe 10 mwezi huu wa Mei.
-
Waraka wa siri wavujishwa: Marekani ilikusudia kuishambulia China kwa silaha za nyuklia
May 23, 2021 06:27Waraka wa siri uliotoroshwa kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) umefichua kwamba, jeshi la Marekani lilitoa pendekezo la kufanya mashambulizi ya anga ya silaha za nyuklia dhidi ya China hapo mwaka 1958 ili kuihami Taiwan mbele ya hujuma yoyote ya majeshi ya utawala wa kikomunisti wa China.
-
Rouhani: Taifa la Iran limeibuka na unshindi katika vita ya kiuchumi
May 23, 2021 06:24Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa taifa la Iran limeibuka na ushindi katika vita ya kiuchumi.
-
Serikali ya Biden yatakiwa iushinikize utawala wa Saudia uondoe mzingiro dhidi ya Yemen
May 21, 2021 21:58Maseneta kadhaa nchini Marekani wamemuandikia barua Rais Joe Biden wa Marekani na kumtaka aishinikize Saudi Arabia ili iondoe mzingiro dhidi ya Yemen. Waliotia saini mapatano hayo ni maseneta Elizabeth Warren na Bernie Sanders.