Maambukizo ya corona yaongezeka sana Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i72774-maambukizo_ya_corona_yaongezeka_sana_marekani
Maambukizi ya virusi vya corona aina ya Delta yamepelekea kuongezeka pakubwa idadi ya wagonjwa na wahanga wa ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 25, 2021 22:08 UTC
  • Maambukizo ya corona yaongezeka sana Marekani

Maambukizi ya virusi vya corona aina ya Delta yamepelekea kuongezeka pakubwa idadi ya wagonjwa na wahanga wa ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani.

Televisheni ya CNN imeripoti kuwa, maambukizi ya corona nchini Marekani yameongezeka kwa asilimia 60, na kwamba kila siku kwa wastani watu elfu 49 wanaambukizwa virusi vya corona nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vifo vya corona pia vimeongezeka kwa asilimia 8 huko Marekani katika siku saba zilizopita na idadi ya vifo inatajwa kufikia watu 272 kwa siku.  

Hii ni katika hali ambayo, wiki kadhaa zilizopita mwenendo wa maambukizi ya corona nchini Marekani ulikuwa katika hali ya kupungua. Marekani inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu walioathiriwa na corona na pia idadi ya vifo vya ugonjwa wa Covid-19. 

Wakati huo huo, Ujerumani pia imeripoti ongezeko la maambukizi ya corona nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti rasmi, hadi sasa zaidi ya watu milioni tatu laki 7 na elfu 61 na 850 wameambukizwa corona nchini humo na wengine zaidi 92 elfu wameaga dunia kutokana na virusi hivyo.  

Ujerumani na mapambano dhidi ya ongezeko la maambukizi ya UVIKO-19