Jul 26, 2021 07:39 UTC
  • Watu 430 wauliwa katika ufyatuaji risasi wiki iliyopita nchini Marekani

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa watu wasiopungua 430 wameuawa katika mashambulizi 915 ya kufyatuana risasi yaliyojiri nchini Marekani wiki iliyopita pekee.

Takwimu hizo zilizotolewa na Taasisi ya Utafiti ya Archive of Violence with Guns kwa kushirikiana na na televisheni ya NBC News zinaonyesha kuwa, watu zaidi ya elfu moja na saba (1007) walijeruhiwa pia katika ufyatuaji huo wa risasi uliofanywa kuanzia tarehe 17 hadi 23 mwezi huu wa Julai huko Marekani. Mwaka jana wa 2020 watu zaidi ya elfu 43 walikuwa wahanga wa vitendo vya mabavu vya kutumia silaha; kiwango ambacho ni cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo miwili ya karibuni huko Marekani. 

Inatabiriwa kwamba, takwimu hizo zitaweka rekodi mpya mwaka huu wa 2021 kwa sababu, idadi ya watu wanaopoteza maisha kutokana na vitendo vya kufyatuliana risasi nchini Marekani imefika zaidi ya elfu 24 hadi sasa tangu mwanzoni mwa mwaka huu. 

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais, Rais Joe Biden wa Marekani aliahidi kwamba atachukua hatua ya kupungua vitendo vya utumiaji silaha katika siku ya kwanza atakapoingia madarakani. Hata hivyo hadi sasa Biden hajachukua hatua ya maana ya kukabiliana na suala hilo. 

Rais Joe Biden wa Marekani 

 

Tags