-
Jibu la suali la leo; kwa nini Albanese anasema hakuna tena mistari myekundu baada ya yeye kuwekewa vikwazo na Marekani?
Jul 13, 2025 07:58Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, ametangaza kwamba uamuzi wa Marekani wa kumuwekea vikwazo unaonyesha kuwa hakuna tena mstari mwekundu wowote.
-
Trump ashadidisha vita vya kibiashara dhidi ya Mexico, EU
Jul 13, 2025 06:04Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuziwekea bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka Mexico na Umoja wa Ulaya ushuru wa asilimia 30 kuanzia Agosti Mosi.
-
Nini madhumuni ya barua mpya ya Iran kwa Baraza la Usalama kuhusiana na uvamizi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Iran?
Jul 13, 2025 02:35Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, na kuwasilisha ripoti iliyosasishwa kuhusu uharibifu uliosababishwa na uvamizi mkubwa wa kijeshi na wa bila ya sababu wa utawala wa Israel dhidi ya Iran.
-
Pentagon yakiri: Kombora la Iran lilitwanga kambi ya US ya Al-Udeid, Qatar
Jul 12, 2025 12:26Katika pigo kubwa kwa heshima ya kijeshi ya Marekani, Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) imekiri kwamba, moja ya makombora ya balestiki ya Iran ilipiga moja kwa moja kambi ya anga ya jeshi la US la Al-Udeid nchini Qatar, wakati wa shambulio la kulipiza kisasi la Tehran mwezi uliopita.
-
Tuhuma dhidi ya Iran zaendelea licha ya Grossi kukiri tena kwamba Iran haitengenezi silaha za nyuklia
Jul 12, 2025 02:34Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesisitiza kuwa, hakuna ushahidi wa kuaminika kwamba Iran imepata silaha za nyuklia na kusisitiza ulazima wa kutatuliwa kidiplomasia suala la nyuklia la Iran.
-
Nigeria: US inazilazimisha nchi za Afrika ziwapokee wakimbizi Wavenezuela
Jul 11, 2025 16:41Nigeria imefichua kuwa Marekani inazishinikiza nchi za bara Afrika kuwakubali wakimbizi wa Venezuela wanaofukuzwa nchini Marekani.
-
Picha za satalaiti zamsuta Trump; Iran ilikiharibu vibaya sana kituo cha US Qatar
Jul 11, 2025 14:44Picha mpya za satelaiti zimefichua uharibifu mkubwa uliotokea katika kituo cha anga cha Marekani cha Al Udeid kilichoko nchini Qatar baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na Iran mwezi uliopita, na hivyo kusuta madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba kambi hiyo kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi haikudhurika.
-
Kuhusu vikwazo vya Trump dhidi yake, Albanese asema mwiba wake ‘umechoma ndipo’
Jul 11, 2025 13:44Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, Francesca Albanese, amesema hakatishwi tamaa na vikwazo alivyowekewa na Marekani. "Inaonekana mwiba umechoma ndipo," amesema Bi Albanese katika kipindi cha mubashara cha televisheni.
-
Unajua kwa nini Marekani imemuwekea vikwazo Ripota Maalumu wa UN kuhusu Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu?
Jul 11, 2025 02:26Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alitangaza Jumatano, Julai 9, kwamba atamuwekea vikwazo Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu, kwa kile alichokiita "juhudi zisizo halali zinazohusiana na uchunguzi wake kuhusu vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza" na eti kwa kuchukua "hatua dhidi ya maafisa wa Marekani na Israel."
-
Zarif aikosoa US kwa kumwekea vikwazo ripota wa UN
Jul 10, 2025 20:24Aliyekuwa Makamu wa Rais katika Masuala ya Kistratajia wa Iran, Mohammad-Javad Zarif amekosoa hatua ya Marekani ya kumuwekea vikwazo Francesca Albanese, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.