-
Wasiwasi waongezeka kuhusu hali mbaya nchini Marekani kufuatia maambukizi ya Corona
Jun 11, 2020 22:05Kuongezeka kwa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Marekani na kufikia zaidi ya waathirika milioni mbili, kumezidisha hali ya wasiwasi nchini humo kuhusiana na kasi ya maambukizi ya virusi hivyo.
-
Vikwazo vya kukaririwa vya Marekani dhidi ya Iran na kufeli mtawalia kwa sera za Washington
Jun 11, 2020 22:00Baada ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Marekani ilianza kutekeleza vikwazo na mashinikizo ya kiwango cha juu ikiwa na lengo la kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kisha kuilazimisha kuketi kwenye meza ya mazungumzo.
-
Waitifaki wa Marekani wapunguza nusu ya askari wao nchini Iraq
Jun 11, 2020 03:30Nchi 29 wanachama wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani nchini Iraq zimepunguza kwa asilimia 50 idadi ya wanajeshi wao vamizi katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Duru mpya ya mazungumzo ya Iraq na Marekani; dalili na matokeo yake
Jun 11, 2020 03:07Mazungumzo kati ya viongozi wa Iraq na Marekani yameanza leo Alkhamisi tarehe 11 Juni.
-
Sisitizo la Borell la kuondoka Marekani JCPOA na madai yasiyo na msingi ya serikali ya Trump
Jun 11, 2020 00:16Rais Donald Trump wa Marekani ni mmoja wa wapinzani wakubwa wa mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na ambaye aliitoa nchi hiyo katika mapatano hayo ya kimataifa tarehe 8 mwezi Mei 2018.
-
Seneta Mmarekani kwa mara nyingine alaani njama za Israel za kupora ardhi zaidi za Wapalestina
Jun 10, 2020 21:52Seneta mmoja wa kujitegemea wa Marekani ametoa onyo kali kuhusu njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kupora ardhi zaidi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusema kuwa, njama hizo zitafuta uwezekano wa kuondoka Wazayuni katika ardhi wanazozikalia kwa mabavu za Wapalestina.
-
Rouhani: Marekani inapanga njama kuzuia kuondolewa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran
Jun 10, 2020 08:24Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kufutwa vikwazo vyote vya silaha dhidi ya Iran baadaye mwezi Oktoba mwaka huu na kusema Marekani imeghadhabishwa na mpango wa kufutwa vikwazo hivyo na sasa inapanga njama ya kutaka vikwazo hivyo visalie.
-
Mazungumzo ya kundi la Taliban na wawakilishi wa Marekani na NATO
Jun 10, 2020 08:16Mullah Baradar, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya kundi la Taliban ameonana na Zalmay Khalilzad, mwakilishi maalumu wa Marekani na Jenerali Austin Scott Miller, kamanda wa wanajeshi wa Marekani na NATO nchini Afghanistan. Mazungumzo hayo yamefanyika katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
-
Maelfu wamuomboleza Floyd huku mashinikizo ya kufanyika mageuzi nchini Marekani yakiongezeka
Jun 09, 2020 08:41Maelfu ya waombolezaji nchini Marekani wametoa heshima zao za mwisho kwa George Floyd aliyefia aliyeuawa na polisi, hatua ambayo imeibua maandamano makubwa kote nchini humo dhidi ya vitendo vya utumiaji mabavu na ubaguzi wa rangi dhidi ya raia wa nchi hiyo wenye asili ya Afrika.
-
Watu zaidi ya 145,000 wataaga dunia kwa corona nchini Marekani hadi kufikia Agosti mwaka huu
Jun 09, 2020 07:17Utabiri wa Chuo Kikuu cha Washington unaonyesha kuwa, idadi ya watu watakaopoteza maisha kwa maambukizi ya corona nchini Marekani hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu itakuwa zaidi ya 145,000.