-
China yayawekea vikwazo makampuni matano ya Marekani kwa kuiuzia silaha Taiwan
Jan 08, 2024 03:09Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza vikwazo dhidi ya makampuni matano ya Marekani kwa kuiuzia Taiwan silaha.
-
Maafisa wa Intelijensia wa Marekani: Israel haitaweza kushinda vita dhidi ya Hizbullah
Jan 08, 2024 02:47Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, tathmini ya siri iliyofanywa na Shirika la Ulinzi wa Intelijensia la Marekani (DIA) imegundua kwamba "itaviwiya vigumu kufanikiwa" vikosi vya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vya medani mbili dhidi ya Hamas huko Gaza na Hizbullah huko Lebanon.
-
Kundi la BRICS ni jukwaa la nchi wanachama kufanya biashara bila dola ya Marekani
Jan 08, 2024 00:05Afisa moja wa Russia amewasilisha takwimu za uzalishaji na matumizi ya nafaka katika kundi la BRICS, na kubainisha kuhusu uwezo wa kundi hilo kufanya biashara bila kutumia sarafu ya dola ya Marekani.
-
Kufichuliwa pande mpya za uhusiano wa Jeffrey Epstein na wanasiasa wa Magharibi na Mossad
Jan 07, 2024 23:17Nyaraka zinazohusiana na Jeffrey Epstein, bepari na bilionea aliyepatikana na hatia ya biashara ya ngono, zimewekwa hadharani kwa amri ya jaji wa mahakama moja ya Marekani, ambapo zimeanika peupe uhusiano wa siri aliokuwa nao na watu mashuhuri wa nchi hiyo na vile vile shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad.
-
Vyombo vya habari vyafichua uhusiano wa mlanguzi wa ngono wa Marekani na Mossad
Jan 07, 2024 04:42Vyombo mbalimbali vya habari duniani vimefichua maelezo zaidi kuhusu uhusiano wa bilionea na myanyasaji wa kingono wa Kimerekani na shirika la ujasusi la Israel (MOSSAD) na watu maarufu duniani.
-
Kumbukumbu ya mwaka wa 3 tangu baada ya tukio la Januari 6; Ishara ya kufifia demokrasia ya Marekani
Jan 06, 2024 07:22Maadhimisho ya miaka mitatu ya shambulio dhidi ya Bunge la Congress ya Marekani Januari 6, 2021 yamewadia huku wapinzani wawili katika uchaguzi wa rais, ambao ni Rais Mdemocrati, Joe Biden, na mgombea mkuu wa chama cha Republican, Donald Trump, wakishambuliana kwa maneno makali hasa katika kipindi hiki cha kuingia mwaka wa uchaguzi wa rais nchini Marekani.
-
Imam wa Swala ya Jamaa Marekani auawa kwa kupigwa risasi
Jan 05, 2024 04:16Imamu wa Msikiti wa Muhammad huko Newark, katika jimbo la New Jersey nchini Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi mbele ya msikiti huo.
-
Yemen: Marekani na Uingereza zitalipa gharama kubwa kwa kushambulia jeshi letu la wanamaji
Jan 02, 2024 08:07Maafisa wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen wametoa mjibizo kwa shambulio la kijeshi la Marekani na kutangaza kwamba nchi hiyo na Uingereza zitalipa gharama kubwa kwa shambulio hilo la kijeshi zilizofanya dhidi ya Jeshi la Wanamaji la Yemen.
-
Uchaguzi wa urais wa 2024 na kuongezeka hatari ya ugaidi ndani ya Marekani
Jan 01, 2024 23:18Jena Marie Griswold, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jimbo la Colorado nchini Marekani, amesema kuwa ametishiwa maisha mara kadhaa baada ya kuwasilisha malalamiko yaliyopelekea kuondolewa jina la Donald Trump, mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka huu wa 2024 kwenye orodha ya wagombea katika jimbo hilo.
-
Seneta wa chama cha Democrate alaani hatua ya Joe Biden ya kutuma silaha Israel
Jan 01, 2024 02:46Seneta wa chama cha Democrate amelaani hatua ya Rais Joe Biden wa Marekani ya kuutumia silaha mpya utawala wa kibaguzi wa Israel.