-
Azimio la Baraza la Usalama kuhusu Gaza: Ni hatua ya lazima lakini haitoshi
Dec 23, 2023 04:48Ijumaa ya jana, Desemba 22, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuongeza misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ukanda wa Gaza bila kutoa wito wa kusitishwa mapigano. Marekani na Russia, wanachama wawili wa kudumu wa Baraza la Usalama, hazikulipigia kura azimio hilo. Wajumbe wengine 13 wamelipigia kura ya ndiyo.
-
Marekani yaikatisha tamaa Ukraine, onyo la Zelensky
Dec 23, 2023 02:50Kuendelea mvutano kati ya Warepublican na Ikulu ya White House juu ya kupasishwa msaada mpya kwa Ukraine, pamoja na kutoa kipaumbele Washington kwa vita vya Gaza na natija yake kusahaulika vita vya Ukraine, kumepelekea serikali ya Biden kuitahadharisha Kyiv kuhusu uwezekano wa kukatiwa au kupunguziwa kiasi kikubwa cha misaada yake.
-
Utafiti: Aghalabu ya Wamarekani wanapinga Israel kupewa misaada ya kijeshi
Dec 22, 2023 22:58Uchunguzi wa maoni uliofanyika nchini Marekani unaonyesha kuwa, akthari ya wapiga kura nchini humo wanapinga mpango wowote wa Washington kuutumia utawala haramu wa Israel misaada zaidi ya kijeshi.
-
Al-Wefaq: Bahrain imewasaliti Wapalestina kwa kujiunga na muungano wa US
Dec 22, 2023 22:57Chama kikuu cha upinzani nchini Bahrain cha al-Wefaq kimesema hatua ya utawala wa Aal-Khalifa ya kujiunga na muungano wa baharini wa Marekani katika Bahari Nyekundu ni kusaliti kadhia ya Palestina.
-
Guterres: US iifutie Iran vikwazo ili JCPOA iendelee kutekelezwa
Dec 19, 2023 23:35Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Marekani iiondolee vikwazo sekta ya mafuta ya Iran ili makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ambayo Washington ilijiondoa kwayo Mei mwaka 2019 yaendelee kutekelezwa.
-
Sisitizo la Putin la kutoziami nchi za Magharibi
Dec 18, 2023 23:04Siku ya Jumapili, Rais Vladimir Putin wa Russia alikiri katika hotuba isiyokuwa ya kawaida kwamba ni makosa kuzidhania vizuri na kuzitegemea nchi za Magharibi na kufikiria kuwa Russia haina tofauti na nchi hizo. Alisema: Nilidhani kimakosa kuwa hakungekuwepo mzozo kati ya Russia na nchi za Magharibi na kwamba ulimwengu ulikuwa umebadilika.
-
Washington Post: Marekani imetengwa kwa kuiunga mkono Israel
Dec 17, 2023 06:26Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, himaya na uungaji mkono kamili wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeifanya Washington kuwa chini ya mashinikizo ya ndani na nje ya Marekani.
-
Kambi ya jeshi ya Ain al-Asad ya US huko Iraq yashambuliwa kwa droni
Dec 15, 2023 07:53Kwa mara nyingine tena, wanamuqawama wa Kiislamu wa Iraq wamewashambulia kwa ndege isiyo na rubani (droni) wanajeshi wa vikosi vamizi vya Marekani katika kambi ya Ain al Asad huko Iraq.
-
Kuidhinishwa kuanza rasmi uchunguzi wa kumsaili Biden katika Bunge la Wawakilishi la Marekani
Dec 14, 2023 23:26Bunge la wawakilishi la Marekani jana Jumatano lilipasisha azimio kwa kura 221 za ndio mkabala wa 212 za kupinga kuanzisha rasmi uchunguzi wa kumsaili Rais Joe Biden wa nchi hiyo. Kabla ya kura hiyo, Kelly Armstrong, Mwakilishi wa Kongresi ya Marekani kwa niaba ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, alichapisha rasimu ya azimio kwa ajili ya kuendelea uchunguzi huo tajwa kwa lengo la kumuuzulu Rais Joe Biden wa Marekani.
-
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Marekani: Mahakama ya Kimataifa ya Haki ni mtumwa wa Marekani
Dec 13, 2023 01:57Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Marekani amesema Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kwa sehemu kubwa ni mtumwa wa Marekani.