Dec 20, 2023 03:05 UTC
  • Guterres: US iifutie Iran vikwazo ili JCPOA iendelee kutekelezwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Marekani iiondolee vikwazo sekta ya mafuta ya Iran ili makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ambayo Washington ilijiondoa kwayo Mei mwaka 2019 yaendelee kutekelezwa.

Mkuu wa Masuala ya Siasa wa Umoja wa Mataifa, Rosemary DiCarlo ameliambia Baraza la Usalama la umoja huo kuwa, Antonio Guterres bado anaitakidi kuwa, JCPOA ndiyo dawa mjarabu ya kuupatia ufumbuzi mvutano juu ya mradi wa nyuklia wa Tehran. 

Guterres alisema katika ripoti yake ya 15 kuhusu azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la umoja huo kwamba: Mapatano ya JCPOA lingali chaguo bora zaidi.

Bi DiCarlo ameeleza kuwa, msimamo wa Guterres ni kwamba Marekani inapasa kuiondolea Iran vizingiti vya kuuza mafuta yake, ili mapatano ya kimataifa ya JCPOA yaendelee kutekelezwa kikamilifu.

Mkuu wa Masuala ya Siasa wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa: Kufanikiwa au kufeli JCPOA, hususan wakati huu hasasi kwa amani na usalama wa dunia, ni jambo zito kwetu sote.

Hivi karibuni pia, Sergei Ryabkov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alisema kuwa, mustakabali wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA upo mikononi mwa Marekani na nchi za Ulaya, huku akitilia shaka azma ya Wamagharibi ya kuyahuisha mapatano hayo kikamilifu.

Suala la Iran kufungamana na majukumu yake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA limethibitishwa katika ripoti 16 za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). 

Tags