Pars Today
Waziri Mkuu wa Ethiopia ametahadharisha kuwa, nchi hiyo itakusanya mamilioni ya wapiganaji iwapo italazimika kingia vitani na Misri katika mzozo wa ujenzi wa bwawa la El Nahdha juu ya maji ya Mto Nile.
Serikali ya Libya imewahamishia nchini Misri makumi ya wahamiaji haramu wanaodaiwa kuwa na magonjwa ya kuambukiza.
Rais wa Misri Abdel-Fatah al-Sisi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wamesisitiza umuhimu wa kuondoa vizuizi vyote vinavyokabili mazungumzo ya pande tatu juu ya Bwawa la GERD linalojengwa na Ethiopia kwenye Mto Nile.
Wizara ya Elimu ya Misri imetoa amri ya kuwafuta kazi walimu 1070 kwa tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la Ikhwanul Muslimin. uamuzi huo umetolewa kufuatia maandamano ya hivi karibuni nchini humo dhidi ya serikali ya Abdel Fattah al Sisi.
Mwanaharakati na mpinzani wa Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri ameanzisha kampeni ya Hashtagi katika mtandao wa kijamii wa Twitter ya kumpiga mnada kiongozi huyo kwa thamani haba na duni.
Kasisi wa kanisa moja nchini Misri, mfuasi wa rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah el Sisi ametoa matamshi ya ajabu ya kumsifu kupindukia rais huyo licha ya kwamba ana kashfa nyingi za wizi, mauaji ya watu na maadili maovu.
Serikali ya Misri imesema mazungumzo mapya kati ya nchi hiyo na Ethiopia kuhusu bwawa la al-Nahdhah linalojengwa na Addis Ababa yamegonga mwamba.
Leo ni Jumapili tarehe 7 Mfunguo Tano Swafar 1441 Hijiria, sawa na tarehe 6 Oktoba 2019 Miladia.
Kamisheni ya Haki na Uhuru ya Misri imetangaza kuwa, askari usalama wa nchi hiyo wamewatia nguvuni raia zaidi ya elfu 3 katika maandamano ya wiki mbili za hivi karibuni dhidi ya Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi huyo.
Spika wa Bunge la Misri amemfananisha Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi hiyo na dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler.