Sep 26, 2019 10:45
Katika hali ambayo, Rais Donald Trump wa Marekani alimtaja Rais Abdul-Fattah al-Sisi wa Misri walipokutana mjini New York makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa, 'Kiongozi Mkubwa', maandamano dhidi ya serikali ya Cairo yameendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ya Kiarabu.